Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Gulamhussein Remtullah, amewataka Madiwani kushirikiana na wataalamu wa Halmashauri katika kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unafanyika kwa ufanisi ili kufikia kwa asilimia 100 bajeti ya Shilingi bilioni 12 iliyowekwa na Halmashauri.
Mstahiki Meya ameyasema hayo jana, Septemba 2, 2026, wakati akifunga kikao cha siku ya kwanza cha Baraza la Madiwani cha Robo ya Nne, kilichofanyika katika Ukumbi Mpya wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.

Aidha, Gulamhussein amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Waheshimiwa Madiwani pamoja na wataalamu wa Halmashauri, akieleza kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kuhakikisha malengo ya Halmashauri yanafikiwa.
Amesema ushirikiano huo ukiendelea kuimarishwa, Halmashauri itaendelea kuwa na utulivu, kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu na hatimaye kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi wa Manispaa ya Tabora.



Discussion
Reader comments
0 contributions