Skip to main content

TABORA: KALUNDE WAJITOLEA NGUVUKAZI UJENZI SHULE YA MSINGI, MEYA AWAPA PONGEZI

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Gulamhussein D. Remtullah, amewapongeza wananchi wa Kata ya Kalunde kwa kujitolea nguvu kazi katika ujenzi wa Shule ya Msingi Msangi A, akieleza kuwa ushiriki wa wananchi ni chachu muhimu katika kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

TABORA: KALUNDE WAJITOLEA NGUVUKAZI UJENZI SHULE YA MSINGI, MEYA AWAPA PONGEZI
Studio Narration JAMBO FM

TABORA: KALUNDE WAJITOLEA NGUVUKAZI UJENZI SHULE YA MSINGI,...

0:00 --:--

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Gulamhussein D. Remtullah, amewapongeza wananchi wa Kata ya Kalunde kwa kujitolea nguvu kazi katika ujenzi wa Shule ya Msingi Msangi A, akieleza kuwa ushiriki wa wananchi ni chachu muhimu katika kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Remtullah ametoa pongezi hizo wakati Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ilipotembelea eneo la ujenzi wa shule hiyo kwa ajili ya kukagua maendeleo ya mradi, ambao kwa sasa umefikia hatua ya uchimbaji wa msingi.

Amesema ushirikiano unaooneshwa na wananchi katika kutekeleza mradi huo ni mfano mzuri wa uwajibikaji na uzalendo katika kuboresha huduma za kijamii, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kushiriki katika shughuli zinazolenga kuimarisha sekta ya elimu.

Aidha, ameeleza kuwa kukamilika kwa shule hiyo kutasaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia, pamoja na kusogeza huduma za elimu karibu zaidi na wanafunzi wa Kata ya Kalunde na maeneo jirani.

Ziara hiyo ya Kamati ya Fedha na Utawala ni sehemu ya juhudi za Halmashauri ya Manispaa ya Tabora katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kutathmini hatua zilizofikiwa na kuhakikisha inatekelezwa kwa kuzingatia malengo yaliyowekwa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.