Na Saada Almasi, Bariadi - Simiyu.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoani Simiyu limetoa angalizo kwa Taasisi Binafsi ,za Umma pamoja na watu binafsi ambao ni watumiaji wa huduma hiyo mkoani humo kuhakikisha wanalipa bili zao mapema na si kuweka malimbikizo kwani kwa kuendelea kufanya hivyo watasababisha shirika hilo kuwasitishia huduma
Akiwa katika ukaguzi wa kituo cha kupozea umeme kinachojengwa katika mtaa wa Imalilo mjini Bariadi mkoani Smiyu ambacho kwa sasa kipo katika asilimia 46 ya ukamilifu wake wa awamu ya kwanza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Lazaro Twange amesema kuwa shirika hilo linategemea mapato kutoka kwa wateja wake hivyo kuchelewa kulipa kunaathiri huduma kwa wananchi wengine.
“unapotumia umeme ujue una wajibu wa kulipa kwani hatuna chanzo kingine cha mapato isipokuwa malipo ya watumiaji kwa hiyo niwaombe taasisi zote na watu binafsi kama unajua unatumia huduma hii basi lipa kwa wakati vinginevyo tutalazimika kusitisha huduma kwako na deni ulipe kisha tunawaunganishia umeme wengine wanaohitaji huduma zetu,wapo wengi”amesema Lazaro
Kituo cha kupozea umeme kimejengwa mahususi kwa ajili ya kupambana na changamoto zikiwemo cha kukatika katika kwa umeme katika mkoa wa Simiyu na Mara kutokanana umeme unaotumika sasa kutoka mkoani Shinyanga ambapo ni mbali hali inayosababisha hitilafu za mara kwa mara wakati wa kusafirishwa.

“tatizo la kukatika katika kwa umeme limekuwa la muda mrefu na mmelalamika sanana mmesikika sasa kituo hiki kinakwenda kuwa suluhisho la changamoto hiyo ili muendelee kufanya shughuli zenu kwa amani kwa sababu serikali ya awamu ya sita tayari imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 7 kuhakikisha njia ya kituo hiki kinajengwa ”ameongeza Lazaro
Akitoa taarifa ya mradi huo wa kupozea umeme Daniel Kato ambaye ni msimamizi wa mradi amesema kuwa hadi kufikia Mei 30 2026 awamu ya kwanza ya maradi huo utakuwa imekamilika hivyo wananchi wajiandae na huduma zilizoboreshwa zaidi
“lengo la mradi huu ni kuweza kuwa na umeme wa uhakika katika mkoa wa Simiyu,Mara na maeneo jirani na kwa awamu ya kwanza ambayo tuna transfoma moja tunatarajia kukamilisjha Mei 30 na baada ya hapo tutaanza awamu ya pili kwa kuongeza transfoma nyingine na kifaa cha kudhibiti umeme hivyo wananchi wategemee umeme wa uhakika,“ amesema Daniel
Ujenzi wa kituo cha kupozea umeme wa Kilovolt 220 kutoka Ibadakuli Shinyanga unajengwa mkoani Simiyu na serikali kwa gharama ya shilingi Bilioni 7 ambapo kukamilika kwake kunakwenda kuleta afueni kwa watumiaji wa huduma hiyo kibiashara na hata kuokoa vifaa vyao vinavyopata hitilafu za mara kwa mara ,japokuwa kwa upande wa wananchi wameendelea kusisitiza ahadi za Mei 30 zitimie ili waepukane na adha hizo.
Discussion
Reader comments
0 contributions