Spika wa Bunge la Seneti la Kenya, Amason J. Kingi, EGH, akipokea maelezo kuhusu safari ya Tanzania katika demokrasia na mchango wake katika kukuza amani na usalama barani Afrika na duniani, alipotembelea Banda la “Karibu Tanzania” katika Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), unaofanyika jijini Arusha.

Akiwa katika Banda hilo, Kingi alipata fursa ya kufahamu hatua mbalimbali zilizopigwa na Tanzania katika maendeleo, hususan katika sekta za miundombinu, afya, elimu na usawa wa kijinsia, pamoja na utekelezaji wa Ajenda ya 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na mwelekeo wa kimkakati wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
WAKATI HUOHUO
Spika wa Bunge la Maldives, Abdul Raheem Abdulla, naye amekuwa ni miongoni mwa wageni waliotembelea Banda la “Karibu Tanzania” katika Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), unaofanyika jijini Arusha.

Akiwa katika banda hilo, Abdulla amepata fursa ya kufahamu safari ya Tanzania katika demokrasia na maendeleo, huku akieleza kufurahishwa na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo Reli ya Kisasa (SGR), Bwawa la Julius Nyerere, Daraja la Busisi (Magufuli), uendelezaji wa Bandari ya Dar es Salaam, pamoja na miundombinu inayoandaliwa kwa ajili ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
#IPU153Tanzania
Discussion
Reader comments
0 contributions