Skip to main content

SOKO AWATAKA WANANCHI KUTUNZA MIUNDOMBINU YA BARABARA MAJENGO

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

SOKO AWATAKA WANANCHI KUTUNZA MIUNDOMBINU YA BARABARA MAJENGO

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

Diwani wa kata ya Majengo, Zacharia Soko ameendelea na zoezi la uboreshaji wa barabara za mitaa katika maeneo mbalimbali
ya taasisi za serikali na kuwataka wananchi kuendelea kutunza barabara hizo.

Katika awamu hii, Soko amekwangua barabara korofi katika Shule ya msingi Majengo kufutia ombi la mkuu wa Shule hiyo alilolitoa hivi karibuni kwa diwani huyo.

Akiwa katika eneo hilo, Soko amesema kuwa ameendelea kutekeleza ahadi zake kwa kukarabati barabara mbalimbali za mitaa ambazo zimekuwa kero kwa wananchi.

"Mitaa mingi ya kata ya majengo imekuwa na barabara nyingi ambazo ni mbovu,nimeendelea kutekeleza ahadi zangu kwa wananchi kuhusu kukarabati barabara za mitaa na leo tuko hapa shule ya msingi majengo," amesema.

Soko amewataka wananchi wa kata ya Majengo kuendelea kuwa na subira na kwamba atahakikisha maeneo yote yenye barabara mbovu yatafikiwa na kukarabatiwa.

"Dhamira yangu ni kuhakikisha kuwa kata ya Majengo inakuwa na miundombinu mizuri ya barabara,hivyo niwaombe wananchi wawe na subira kwani tumejipanga kufikia maeneo yote yenye changamoto ya barabara," ameongezea Soko.

Katika hatua nyingine, Soko ametoa rai kwa wananchi wa kata ya majengo na watumiaji wengine wa barabara kuendelea kuzitunza barabara hizo na kuacha tabia ya kupitisha mifugo na kutupa taka kwenye mitaro.

"Barabara zetu tukizitunza zitadumu sana,hivyo wananchi tuache tabia ya kupitisha mifugo pamoja na kutupa taka ngumu kwenye mitaro hali inayosababisha mitaro kuziba na maji kubadili uelekeo matokeo yake yanasabisha mafuriko," amesisitiza Soko.

Nao baadhi ya wananchi wa kata ya Majengo wamemshukuru Soko kwa kuendelea kutatua changamoto mbalimbali katika kata hiyo.

"Tunashukuru sana Mh.Soko kwa kuendelea kuwa karibu na wananchi na kutatua changamoto mbalimbali zinazotusumbua wananchi,tunamuombea azidi kuendelea hivi hivi ili kuleta mabadiliko katika kata yetu" Wamesema wanachi hao.

Sambamba na hayo wananchi wametoa ombi kwa diwani huyo kuzidi kuimarisha ulinzi katika mitaa ya majengo kwani bado kuna vibaka wanaosumbua nyakati za usiku.

"Ombi letu kwa Mheshimiwa Diwani,tunaomba aimarishe swala la ulinzi katika mitaa yetu,kumekuwa na vijana ambao wanasumbua wananchi nyakati za usiku hivyo ulinzi ukiimalisha tunaimani tutaishi kwa raha sisi na mali zetu,", walielezea Wananchi hao.

Kata ya Majengo manispaa ya Kahama ni kata ambayo ipo ukanda wa maji kutokana na hali ya kijiografia hali inayosababisha maji kutumana sana wakati wa masika.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.