Skip to main content

SIRRO AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA WAPYA AKIWATAKA KUTATUA KERO ZA WANANCHI

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amewataka Wakuu wa Wilaya wapya kuhakikisha wanawatumikia wananchi kwa kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo kutatua migogoro ya ardhi, kudhibiti uhamiaji haramu na kuziwezesha sekta binafsi kukua ili kufikia dira ya maendeleo ya taifa ya 2050.

SIRRO AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA WAPYA AKIWATAKA KUTATUA KERO ZA WANANCHI
Studio Narration JAMBO FM

SIRRO AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA WAPYA AKIWATAKA KUTATUA KERO...

0:00 --:--

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amewataka Wakuu wa Wilaya wapya kuhakikisha wanawatumikia wananchi kwa kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo kutatua migogoro ya ardhi, kudhibiti uhamiaji haramu na kuziwezesha sekta binafsi kukua ili kufikia dira ya maendeleo ya taifa ya 2050.

Balozi Sirro amesema hayo wakati wa kuwaapisha Wakuu wa Wilaya wapya ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo.

Sirro amesema uongozi ni kuwaunganisha wananchi kwa kutatua changamoto zao bila kujali itikadi za vyama vyao vya kisiasa.

Wakati huohuo Sirro amezitaja baadhi ya changamoto ambazo zipo kwenye Wilaya hizo ambazo angependa kuona zikitatuliwa na Wakuu hao wa Wilaya ikiwemo uhamiaji haramu, wizi wa zana za uvuvi katika Ziwa Tanganyika na kutatua migogoro ya ardhi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma Jamal Tamimu amesema wakuu wa Wilaya ya Kigoma waliopita wamefanya kazi ambayo imeleta matokeo chanya ikiwemo usimamizi wa miradi ya maendeleo na imepelekea wananchi kukiamini Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa Wilaya, Mkuu wa Wilaya mpya wa Uvinza ambaye ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema atahakikisha anafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kikamilifu na kusimamia suala la ulinzi na usalama ili wananchi waweze kufanya kazi za maendeleo kwa utulivu.

Uapisho huo wa Wakuu wa Wilaya umefanyika baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.