Skip to main content

SIRI NZITO: MACKENZIE ATEKELEZA VIFO AKIWA GEREZANI

Fukuto la kesi ya mauaji ya watu zaidi ya 400 inayomkabili mchungaji Paul Nthenge Mackenzie linazidi kutokota, mara baada ya mfungwa anayefahamika kwa jina la Kalume Kitsao Rimba anayetumikia kifungo cha miaka 50 jela kuieleza mahakama jinsi alivyojihusisha na utekelezwaji wa mauaji kupitia laini mbili za simu ndani ya gereza hilo lililoko mjini mombosa.

SIRI NZITO: MACKENZIE
ATEKELEZA VIFO AKIWA GEREZANI
Studio Narration JAMBO FM

SIRI NZITO: MACKENZIE ATEKELEZA VIFO AKIWA GEREZANI

0:00 --:--

Fukuto la kesi ya mauaji ya watu zaidi ya 400 inayomkabili mchungaji Paul Nthenge Mackenzie linazidi kutokota, mara baada ya mfungwa anayefahamika kwa jina la Kalume Kitsao Rimba anayetumikia kifungo cha miaka 50 jela kuieleza mahakama jinsi alivyojihusisha na utekelezwaji wa mauaji kupitia laini mbili za simu ndani ya gereza hilo lililoko mjini mombosa.

kwa mujibu wa maelezo laini hizo zinadaiwa kutumiwa na Paul Mackenzie kuwasiliana na watu waliokuwa nje ya gereza kwa kutuma na kupokea pesa akiwa chini ya kizuizi.

katika maelezo yake ameitanabaishia Mahakama kwamba japo simu za mkononi na vifaa vingine vya mawasiliano havipati kibali gerezani, walakini alipoanza kutumikia kifungo chake alikuta wafungwa waliowengi wakivitumia kimagendo.

aliendelea kukiri kwamba mabadiliko ya uongozi wa gereza yalileta hatua kali zaidi za kiusalama, huku wasimamizi wapya wakifanya upekuzi wa kina na kukamata bidhaa zilizopigwa marufuku.

katika maelezo yake ya kujitetea kitsao anaeleza simu kuiacha nyumbani huku laini hizo mbili akizibeba hadi alipofikishwa gerezani.

kitsao alisema maafisa wa gereza walipekua chumba chake gerezani mnamo septemba 20, 2025, na kuchukua biblia mbili pamoja na kipande cha karatasi kilichokuwa na majina na nambari za simu.

aidha siku iliyofuata, maafisa walifanya upekuzi mwingine na kubaini uwepo wa laini mbili, moja iliyosajiliwa kwa jina lake na nyingine kwa jina la mkewe, tatu safari.baadaye, polisi walimfahamisha kuwa laini yake ilikuwa imewekwa kwenye simu ambayo ilishukiwa kutumiwa na mackenzie kuhusiana na makosa ya jinai yaliyokuwa yakifanyiwa uchunguzi.

kitsao alikiri kumfaham mackenzie kupitia taarifa za habari kuhusu vifo vya wafuasi wake huko shakahola.

hata hivyo, alikiri kwamba mara kwa mara alikuwa akimpa mfungwa mwenzake charles kalume mojawapo ya laini zake.

kwa mujibu wa kitsao, charles alikuwa akiomba simu kutoka kwa wafungwa wengine.

“charles ndiye aliye katika nafasi nzuri zaidi ya kueleza kwa sababu ndiye mtu pekee ambaye nimempa laini yangu ya simu,” aliiambia mahakama.

sajenti stanslous bongo chikute, afisa anayesimamia upekuzi katika gereza la shimo la tewa, aliimbia mahakama kuwa hakuweza kubaini iwapo maafisa wa gereza walihusika katika kupenyeza laini hizo, akisema kitsao ndiye aliyekuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kueleza jinsi alivyoviingiza ndani ya gereza.

kadharika katika chumba cha gereza cha mackenzie, maafisa walisema walipata laini tatu za airtel zilizokuwa zimefichwa ndani ya vijiti vya kunyoa ndevu vilivyokuwa sakafuni.

polisi pia walipata daftari lililokuwa na majina na nambari za simu, ambazo baadhi zilikuwa zimeandikwa juu ya maandishi mengine ili kuzifanya kutosomeka vyema, pamoja na maandishi yaliyoandikwa kwa mkono, yakiwemo karatasi moja iliyokuwa na jina emily ayugi, na biblia.

mchungaji paul mackenzie wa kanisa la good news international church anadaiwa kusababisha vifo vya zaidi ya watu 400, huku ikiwa hadi sasa miili zaidi ya 429 imefukuliwa katika msitu wa shakahola, kaunti ya kilifi, nchini kenya.

katika kesi ya kwanza ya mauaji iliyokamilika, paul mackenzie pamoja na washtakiwa wenzake 28 wamepatikana na hatia ya kuua jumla ya watu 191.

kwa mujibu wa ripoti za uchunguzi mackenzie alitumia mbinu mbalimbali za kisaikolojia, kimafundisho na kimabavu kuwalazimisha na kuwashawishi waumini wake kujinyima chakula hadi kufa katika msitu wa shakahola

miongoni mwa mbinu zilizoainishwa na chunguzi hizo ni pamoja na mafundisho makali ya itikadi kali yaani (brainwashing)

mackenzie alitumia mbinu hii akiwahubiria waumini wake kuwa mwisho wa dunia unakaribia na njia pekee ya "kwenda mbinguni moja kwa moja kukutana na yesu" kabla ya kiama ilikuwa ni kufunga kula na kunywa hadi kufa akienda mbali zaidi na kuwajengea hofu kubwa kuhusu maisha ya duniani na mifumo ya kisasa

pili mfumo wa "mlolongo wa vifo" yaani (structured hierarchy of death) waendesha mashtaka walibainisha kuwa mackenzie aliweka utaratibu maalum wa nani anapaswa kuanza kufunga na kufa kwanza ambapo walioanza walikuwa ni watoto, wakifuatiwa na vijana.

kisha walifuata wanawake, na mwisho kabisa walipaswa kuwa wanaume.

hali hii ilisababisha watoto wengi (zaidi ya watoto 190) kuwa wahanga wakuu kwa kunyimwa chakula huku wazazi wao wakishurutishwa kushuhidia.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.