Skip to main content

SINGIDA WAZINDUA RASMI KAMPENI CHANJO YA POLIO, WATOTO 99,714 KUFIKIWA

Na Saulo Stephen - Singida.

SINGIDA WAZINDUA RASMI KAMPENI CHANJO YA POLIO, WATOTO 99,714 KUFIKIWA

Na Saulo Stephen - Singida.

Halmashauri ya Wilaya ya Singida Mkoani Singida imezindua rasmi kampeni ya utoaji wa chanjo ya Polio yenye lengo la kuwafikia watoto 99,714 walio na umri chini ya miaka 10, ili kuwalinda dhidi kirusi hatari cha Polio kinachoweza kusababisha Ulemavu wa kudumu au kupelekea Vifo kwa Watoto.

Uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika katika Kituo cha Afya Ilongero, Halmashauri ya Wilaya ya Singida na Kuzinduliwa na Katibu tawala wa Wilaya hiyo Bi.Naima Chondo akimuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Singida Godwin Gondwe.

Akizungumza katika hafla hiyo, Chondo amewahimiza wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kupata chanjo hiyo muhimu, huku akisisitiza kuwa ugonjwa wa Polio hauna tiba hivyo kinga ndiyo njia pekee ya kuwalinda watoto dhidi ya ugonjwa huo.

Aidha kampeni hiyo itafanyika kupitia vituo vya afya, shule, huduma za nyumba kwa nyumba pamoja na maeneo yenye mikusanyiko ya watu kama vile masoko na stendi za mabasi ili kuhakikisha hakuna mtoto anayekosa chanjo.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Dkt. Dorisila Mlenga John, amemshukuru Katibu Tawala wa Wilaya kwa kuzindua kampeni hiyo na kubainisha kuwa elimu ya kutosha tayari imetolewa kwa wananchi.

Kampeni hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya chanjo ya matone aina ya nOPV2, inayotarajiwa kufanyika kwa siku nne kuanzia Machi 24 hadi 27, 2026 ambapo kwa Wilaya ya Singida inajumuisha upatikanaji wa dozi 124,500 za chanjo, vifaa tiba vya kutosha pamoja na mafunzo kwa wasimamizi pamoja na watoa huduma za afya.

Katibu tawala Wilaya ya Singida, Bi. Naima Chondo akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya Polio Singida DC.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.