Skip to main content

SINGIDA WAJADILI KUIMARISHA UWAJIBIKAJI, USIMAMIZI FEDHA ZA UMMA

Na Saulo Stephen - Singida.

SINGIDA WAJADILI KUIMARISHA UWAJIBIKAJI, USIMAMIZI FEDHA ZA UMMA

Na Saulo Stephen - Singida.

Kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama cha kujadili na kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2025/2026, kimetoa msisitizo wa kuimarisha uwajibikaji katika usimamizi wa fedha za umma na kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano Halimashauri ya Mkalama, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amezitaka halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha zinalipa madeni yote ndani ya kipindi cha miaka miwili, huku zikiongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kufunga hoja za CAG.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego.

Dendego amesema viongozi wa kimkakati wanapaswa kuongoza mabadiliko kwa vitendo, akieleza kuwa Mkoa wa Singida umejipanga kuongeza kasi ya utendaji ili kuhakikisha hoja za ukaguzi zinapungua na kubaki kwenye kiwango cha tarakimu moja.

"Pale tulipokuwa tunatembea sasa tuanze kukimbia. Maendeleo si lelemama; lazima tuongeze kasi, tulipe madeni, tufunge hoja na tufikie malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050," amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Moses Machali.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Moses Machali, amesema viongozi hawapaswi kuficha changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu yao, akisisitiza kuwa uwazi husaidia kupata suluhisho na kuboresha utendaji wa halmashauri.

Amesema hoja za CAG zinapaswa kutazamwa kama fursa ya kuboresha mifumo ya usimamizi wa fedha na miradi ya maendeleo badala ya kuziona kama adhabu, huku akiwataka watendaji kushirikiana kurekebisha mapungufu kwa wakati.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Mohamed Hamis.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Mohamed Hamis, amewataka viongozi na wananchi kuacha kutegemea fedha kutoka Serikali pekee katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, akisisitiza matumizi bora ya rasilimali zilizopo na kuhamasisha urejeshaji wa mikopo ya asilimia 10 ili wananchi wengi zaidi wanufaike.

Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bi. Asia Juma Mesos, amesema halmashauri hiyo imefanikiwa kupunguza hoja za CAG kutoka 61 hadi 9, hatua inayoonyesha kuimarika kwa uwajibikaji na usimamizi wa fedha za umma.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bi. Asia Juma Mesos.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.