Wazazi na walezi mkoani Singida wametakiwa kuwafuatilia watoto kwa karibu na kuwazuia kucheza kwenye madimbwi, mifereji na mito wakati wa mvua za El Niño, ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amesisitiza umuhimu wa wananchi kuchukua tahadhari za usalama, huku akiwahimiza wakulima kutumia mvua hizo kwa uzalishaji wa chakula na kuongeza mavuno.
Amesema wananchi wanapaswa kumuomba Mungu awajalie mvua za kiasi zisizo na madhara, lakini pia kutimiza wajibu wao kwa kuchukua hatua za kujilinda, hususan kuhakikisha watoto wanakuwa salama wakati maji yanapoongezeka katika maeneo yao.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego.
Aidha, amebainisha kuwa Mkoa wa Singida una fursa ya kutumia mvua hizo kuongeza uzalishaji wa chakula na kusaidia maeneo mengine yanayoweza kukumbwa na changamoto za uzalishaji kutokana na hali ya hewa.
Discussion
Reader comments
0 contributions