Na Saulo Stephen - Singida.
Mkoa wa Singida umefikia asilimia 70 ya utoaji chanjo ya polio kwa watoto walio na umri chini ya miaka 10 huku jumla ya watoto laki 710,623 wakitarajiwa kufikiwa na chanjo hiyo mpaka kukamilika kwa zoezi hilo.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego wakati akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa chanjo hiyo ngazi ya mkoa, uzinduzi ambao umefanyika katika viwanja vya Hospitali ya Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.

Amsema asilimia hiyo 70 ni mpaka kufikia leo machi 26, 2026 ambapo, zoezi hilo limeanza rasmi machi 24, 2026 huku likitarajiwa kufika tamati machi 27, 2026 katika mkoa wa Singida, ambapo kwa Wilaya ya Manyoni tayari mpaka sasa wamsehachanja watoto chanjo hiyo kwa asilimia 82, huku matarajio ya mkoa nikuhakikisha watoto wote waliolengwa wanapatiwa chanjo dhidi kirusi hatari cha Ugonjwa wa Polio.
Aidha, RC Dendego amempongeza Mganga mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Victorina Ludovick pamoja na timu yake kwa namna ambavyo wamekuwa wakipambana kwa vitendo katika kufanikisha zoezi hilo la chanjo kuanzia mjini mpaka vijijini, huku pia akitoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Singida kuendele kuwapeleka watoto kupata chanjo pamoja na kuwakumbusha kunawa miko na maji tiririka ili kujikinga na maambukizi ya magonjwa mbalimbali ukiachana na Ugonjwa wa polio.

Hata hivyo amewasisitiza wananchi wa mkoa wa Singida kuzingatia matumizi ya vyoo bora ili kuepukana na magonjwa ya Mlipuko ikiwemo polio ambayo kirusi chake kimebainika kupatikana katika maji taka .
Awali akizungumza katika uzinduzi wa Chanjo hiyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Victorina Ludovick amesema huduma zote za utoaji chanjo zinaendelea kutolewa katika halimashauri zote saba za Mkoa huo huku chanjo zikiwa za kutosha pamoja na vifaa vyote vinavyohitajika katika utoaji huduma, vilevile akiwapongeza wananchi kwa namna ambavyo wameendelea kutoa ushirikiano wa kuwapeleka watoto kupata chanjo toka kuanza kwa zoezi hilo Machi 24,2026.
Discussion
Reader comments
0 contributions