Takribani Watu saba wamefariki dunia na wengine 17 kujeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Senkenke, wilayani Iramba mkoani Singida, baada ya Lori kupata hitilafu ya mfumo wa breki na kuligonga kwa nyuma basi dogo aina ya Coaster.
Ajali hiyo imetokea hii leo Juni 2, 2026 majira ya saa 4:00 asubuhi ambapo Coaster hiyo iligongwa ikitoka Singida kuelekea Igunga mkoani Tabora, kabla ya magari yote mawili kutumbukia kwenye korongo kando ya barabara kuu ya Dar es Salaam–Mwanza.

Akiwa enwo la tukio, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, ametqkq kufanyika uchunguzi wa ajali hiyo, huku akiwatembelea majeruhi waliolazwa hospitalini na kutoa pole kwa familia zilizoathirika.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Peter Luhega amesema, majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu huku baadhi yao wakiwa katika hali ya uangalizi maalumu kutokana na majeraha waliyopata.

Discussion
Reader comments
0 contributions