Skip to main content

SINGIDA NI TAJIRI, INA KILA SABABU YA KUONGEZA MAPATO YA NDANI - RC DENDEGO

Na Saulo Stephen - Singida.

SINGIDA NI TAJIRI, INA KILA SABABU YA KUONGEZA MAPATO YA NDANI - RC DENDEGO

Na Saulo Stephen - Singida.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego amesema, Halmashauri ya Wilaya ya Singida ina kila sababu ya kuwa miongoni mwa Halmashauri tajiri nchini kutokana na wingi wa rasilimali na maeneo ya uwekezaji, akisisitiza kuongeza mapato ya ndani, kuondoa hoja za ukaguzi na kufikia kiwango cha single digits ili kuchochea safari ya kuelekea Jiji la Singida.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani cha kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Dendego amesema maendeleo ni ushindani unaohitaji ubunifu na usimamizi madhubuti wa rasilimali.

Amewataka viongozi kutokuzalisha hoja mpya, kuwachukulia hatua watakaobainika kuwa chanzo cha hoja hizo, huku akisisitiza kuwa Halmashauri hiyo ijikite katika kubuni vyanzo vipya vya mapato, kuharakisha mradi wa Hewa ya Ukaa na kuvutia uwekezaji ili kuongeza pato la wananchi na kuifanya Singida kuwa kinara wa utekelezaji wa Dira ya 2050.

Aidha amesema Serikali itaendelea kupeleka wataalamu wa uwekezaji kupitia Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa ili kutambua na kuendeleza maeneo yenye fursa za kiuchumi, akiwataka viongozi kuacha kushughulikia masuala madogo na kuelekeza nguvu kwenye miradi mikubwa ya kimkakati itakayoiwezesha Singida DC kuwa nguzo ya maendeleo ya Jiji la Singida.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Elia Digha, amesema halmashauri imekusanya asilimia 101 ya mapato na imelenga kufikia bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni nne, huku akiahidi kusimamia kikamilifu maagizo ya Mkuu wa Mkoa pamoja na kuimarisha usimamizi wa mapato na miradi ya maendeleo.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Bi. Ester Chaula, ameahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa ili kuongeza mapato, kupunguza hoja za CAG na kuimarisha uwajibikaji.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.