Skip to main content

SINGIDA: MAAFISA HABARI WAJENGEWA UWEZO MBINU BORA ZA KURIPOTI CHANJO YA POLIO

Na Saulo Stephen - Singida.

SINGIDA: MAAFISA HABARI  WAJENGEWA UWEZO MBINU BORA ZA KURIPOTI CHANJO YA POLIO

Na Saulo Stephen - Singida.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Victorina Ludovick amefungua mafunzo ya siku moja kwa Maafisa Habari wa Mkoa huo, yakilenga kuwajengea uwezo kuhusu chanjo ya polio pamoja na mbinu bora za kuripoti na kutoa elimu kwa jamii.

Akizungumza wakati wa ufunguzi, Dkt. Ludovick amesisitiza umuhimu wa vyombo vya habari katika kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu chanjo ya polio na kusema maafisa habari wana nafasi kubwa ya kusaidia kuondoa upotoshaji na uvumi usio na msingi.

Chanjo ya polio inatarajiwa kuanza kutolewa rasmi kuanzia Machi 24, mwaka huu, katika vituo vyote vya kutolea huduma ndani ya Manispaa ya Singida ambapo huduma hiyo ikitarajia kuwafikia watoto kupitia shule zote za msingi pamoja na maeneo mbalimbali yenye mikusanyiko ya watu ili kuhakikisha kila mtoto anayelengwa anafikiwa.

Ameongeza kuwa lengo ni kuhakikisha watoto wote wenye umri chini ya miaka 10 wanapatiwa chanjo hiyo kwa ajili ya kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa polio.

Hata hivyo Dkt. Ludovick ametoa wito kwa maafisa habari kutumia taaluma yao kuhamasisha jamii kujitokeza kwa wingi, akibainisha kuwa chanjo hiyo ni salama na muhimu katika kulinda afya za watoto.

Aidha amepongeza kuwa mwitikio wa wananchi wa Singida umekuwa mzuri katika kampeni zilizopita, na akaeleza matumaini kuwa kampeni hii pia itapokelewa vyema ili kuzuia ulemavu na vifo vinavyoweza kusababishwa na ugonjwa wa polio.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa, Manispaa ya Singida inalenga kuwapatia chanjo watoto 42,640, ikiwa ni sehemu ya watoto 542,041 wanaotarajiwa kupatiwa chanjo katika Mkoa mzima wa Singida. 

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.