Timu ya Singida Journalist imeibuka na ushindi mnono wa mabao 5-2 dhidi ya TAFCA FC katika mchezo wa kirafiki uliopigwa leo Jumapili Oktoba 25, 2026 katika Uwanja wa CCM Liti mjini Singida.
Mchezo huo ulioanza majira ya saa 3 asubuhi, ulishuhudia ushindani mkubwa tangu dakika za mwanzo, ambapo Singida Journalist walionesha kiwango bora na umahiri wa hali ya juu na kuweza kutawala mchezo kwa kiasi kikubwa na hatimaye kuibuka na ushindi huo mnono.
Mabao hayo matano ni matokeo ya mazoezi na maandalizi mazuri ambayo timu hiyo imekuwa ikiyafanya kwa muda, huku TAFCA FC nao wakionesha upinzani na kupata mabao mawili ya kufutia machozi.
Akizungumza baada ya mchezo huo Nahodha wa kikosi hicho Robert Onesmo, Robertinho "huo, amesema ushindi huo ni chachu kubwa kuelekea michuano inayowakabili.
Baada ya mchezo huo, timu ya Singida Journalist itaendelea kuweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na michezo mbalimbali ya kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano mbalimbali iliyopo mbele yao ikiwemo michuano ya Yagi Kiaratu Jimbo Cup inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Timu hiyo imewataka wadau wa michezo na mashabiki kuendelea kuiunga mkono katika harakati zake za kudumisha mshikamano kupitia michezo.
Discussion
Reader comments
0 contributions