Skip to main content

SINGIDA HATUWEZI VUMILIA VIFO VYA AKINA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO - DKT. FATUMA

Na Saulo Stephen - Singida.

SINGIDA HATUWEZI VUMILIA VIFO VYA AKINA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO - DKT. FATUMA

Na Saulo Stephen - Singida.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatuma Mganga, amesema Mkoa wa Singida hauwezi kuendelea kuvumilia vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga wakati Serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa katika miundombinu, vifaa tiba na wataalamu wa afya, akisisitiza kuwa sasa ni wakati wa kuona matokeo ya uwekezaji huo kwa kupungua kwa vifo hivyo.

Akizungumza wakati wa kikao cha kujadili mikakati ya kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga kilichofanyika katika Ukumbi Mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Mganga alisema vifo vya akina mama na watoto havikubaliki tena na kila mtoa huduma anatakiwa kuwajibika kuhakikisha mama anayefika kituoni anapata huduma bora na salama.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatuma Mganga.

Alisema Serikali imejenga vituo vya afya, hospitali za wilaya, imeajiri watumishi na kununua vifaa vya kisasa, hivyo haiingii akilini kuona miundombinu na rasilimali zikiongezeka huku vifo vikibaki juu. Alisisitiza kuwa kipimo kikubwa cha utendaji wa viongozi na wataalamu wa afya ni uwezo wao wa kupunguza vifo vya mama na mtoto.

“Vifo hivi havikubaliki kabisa Mkoa wa Singida. Yawezekana mkawa na pilikapilika nyingi, lakini kama vifo bado vipo, kazi yote mnayoifanya haina maana. Kinachotufanya tujue mnafanya kazi ni kuona vifo vinapungua na akina mama wanaendelea kuishi,” alisisitiza.

"Sababu nyingi za vifo hivyo zinaweza kuzuilika" - Dkt. Fatuma.

Dkt. Mganga alieleza kuwa sababu nyingi za vifo hivyo zinaweza kuzuilika iwapo huduma za kliniki kwa wajawazito zitatolewa kwa ubora unaotakiwa. Aliwataka RHMT, CHMT na waganga wakuu wa halmashauri kuongeza usimamizi wa huduma za antenatal care, kuhakikisha wajawazito wanapimwa kikamilifu na kupata matibabu mapema wanapoonesha viashiria vya hatari.

“Tusikubali mama kupata changamoto mikononi mwetu. Mama akifika kwenye kituo cha afya, tumieni utaalamu, vifaa na rasilimali zote zilizopo kuhakikisha anaondoka salama pamoja na mtoto wake. Vifo hivi lazima vipungue,” alisema.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Jesca Lebba.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Jesca Lebba, alisema Mkoa umeweka mikakati mbalimbali ya kupunguza vifo hivyo ikiwemo kuanzisha Mama Mwambata, Task Force ya kufuatilia kila kifo kinapotokea, mfumo wa kufuatilia wajawazito.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.