Skip to main content

SIMANZI: KIJANA ALIYEMUUWA JIRANI YAKE KAGERA AJITEKETEZA KWA MOTO3

Na Clavery Christian, Biharamulo - Kagera

SIMANZI: KIJANA ALIYEMUUWA JIRANI YAKE KAGERA AJITEKETEZA KWA MOTO3

Na Clavery Christian, Biharamulo - Kagera

Hali ya simanzi na taharuki imetanda katika Kitongoji cha Chai Taka, Kijiji cha Rugondo, Kata ya Ruziba wilayani Biharamulo mkoani Kagera, baada ya kijana mmoja mwenye umri wa miaka 29 kudaiwa kumuua jirani yake mwenye umri wa miaka 70 kabla ya kujiteketeza kwa moto ndani ya nyumba yake.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 4:00 usiku wa Julai 1, 2026, likiwahusisha marehemu Paschal Ntakimazi (70) na Furaha Charles (29).

Akizungumza kwa masikitiko, mke wa marehemu Paschal Ntakimazi, Alisia Kinama (70), amesema familia yao imepata pigo kubwa kufuatia tukio hilo, akieleza kuwa kijana huyo alidaiwa kumuua mume wake kabla ya kwenda kujifungia ndani ya nyumba yake na kujiunguza hadi kufariki dunia.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Rugondo, Emanuel Sebahutu, amesema tukio hilo limewaacha wananchi katika hofu na majonzi makubwa kutokana na ukatili wake, huku akibainisha kuwa uchunguzi unaendelea kubaini chanzo halisi cha mauaji hayo.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo pia alieleza mazingira yaliyopelekea tukio hilo, akisema lilitokea ghafla na kuwashangaza wakazi wa eneo hilo.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Ruziba, Donard Samsoni, amewataka wananchi kudumisha amani na kutafuta suluhisho la migogoro kwa kufuata taratibu za kisheria badala ya kujichukulia sheria mkononi.

Naye Polisi Jamii wa Kata ya Ruziba, SGT Masele Joseph, amesema tukio hilo linapaswa kuwa fundisho kwa jamii nzima, akisisitiza umuhimu wa kutatua migogoro kupitia vyombo husika na kutoa taarifa mapema kwa mamlaka pale dalili za migogoro zinapoonekana ili kuepusha madhara makubwa kama yaliyotokea.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.