Skip to main content

SIMAI: TUSIYUMBISHWE NA SIASA ZA URAIS 2030, TUMHESHIMU DKT. SAMIA

Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mohamed Simai Said, amewaonya wanaofanya siasa za urais mapema, akisisitiza viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanapaswa kumheshimu Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kuelekeza nguvu katika kuwatumikia wananchi badala ya kuanza makundi ya kisiasa.

SIMAI: TUSIYUMBISHWE NA SIASA ZA URAIS 2030, TUMHESHIMU DKT. SAMIA
Studio Narration JAMBO FM

SIMAI: TUSIYUMBISHWE NA SIASA ZA URAIS 2030, TUMHESHIMU DKT....

0:00 --:--

Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mohamed Simai Said, amewaonya wanaofanya siasa za urais mapema, akisisitiza viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanapaswa kumheshimu Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na kuelekeza nguvu katika kuwatumikia wananchi badala ya kuanza makundi ya kisiasa.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo, Ijumaa Mei 22, 2026 Simai amesema baadhi ya watu wameanza harakati za chinichini kutafuta urais wa 2030, akisema hatua hiyo inaweza kuvuruga umoja ndani ya chama.

Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mohamed Simai Said.

Amesisitiza kuwa wanachama wanapaswa kusimama pamoja nyuma ya Dkt Samia kama mwenyekiti wa chama na alama ya mshikamano wa taifa.

“Tusikubali kuchanganywa kuelekea 2030. Sasa ni muda wa kufanya kazi, kutekeleza ilani na kuhakikisha vijana wanapata ajira,” amesema Simai.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.