Skip to main content

SILAHA, RISASI 23 ZASALIMISHWA NKASI

Silaha moja ya aina ya AK-47 pamoja na risasi 23 imesalimishwa kwa hiari na mtu au watu wasiofahamika katika Wilaya ya Nkasi, Mkoa wa Rukwa. Usalimishaji huu umetokana na elimu inayoendelea kutolewa kupitia kampeni ya usalimishaji wa silaha haramu.

SILAHA, RISASI 23 ZASALIMISHWA NKASI
Studio Narration JAMBO FM

SILAHA, RISASI 23 ZASALIMISHWA NKASI

0:00 --:--

Silaha moja ya aina ya AK-47 pamoja na risasi 23 imesalimishwa kwa hiari na mtu au watu wasiofahamika katika Wilaya ya Nkasi, Mkoa wa Rukwa. Usalimishaji huu umetokana na elimu inayoendelea kutolewa kupitia kampeni ya usalimishaji wa silaha haramu.

Silaha hiyo imesalimishwa Oktoba 19, 2026, katika eneo la wazi la Kijiji cha Lyazumbi, Kata ya Paramawe, ikiwa ni sehemu ya mwitikio wa wananchi katika kuunga mkono kampeni ya usalimishaji silaha haramu iliyozinduliwa Agosti 31,2026 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi.

Kampeni hiyo inaendelea kuhamasisha wananchi kusalimisha kwa hiari silaha wanazomiliki kinyume cha sheria kabla ya kuhitimishwa kwa kipindi cha msamaha Oktoba 31, 2026.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, SACP. Shadrack Masija anawasisistiza wananchi kusalimisha silaha wanazomiliki kinyume cha sheria. Aidha, anawahimiza pia wamiliki wa silaha zilizosajiliwa kisheria ambao wamefariki dunia, wazee sana au wasiokuwa na uwezo wa kuendelea kuzitumia kutokana na umri mkubwa au maradhi, kuzisalimisha kwa ajili ya usalama wa jamii.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.