Skip to main content

SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI: ULINZI, HAKI ZA MTOTO WA KIKE VIWE KIPAUMBELE

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA-ZNZ), kimeungana na wadau wa kutetea haki za watoto katika kuadhimisha siku ya mtoto wa kike Duniani yenye kaulimbiu "Tokomeza Ndoa za Utotoni na Wekeza katika Haki za Wasichana." ambayo huadhimisha kila ifikapo tarehe 11 Oktoba, inayolenga kusisitiza ulinzi na haki za mtoto wa kike.

SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI: ULINZI, HAKI ZA MTOTO
WA KIKE VIWE KIPAUMBELE
Studio Narration JAMBO FM

SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI: ULINZI, HAKI ZA MTOTO WA KIK...

0:00 --:--

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA-ZNZ), kimeungana na wadau wa kutetea haki za watoto katika kuadhimisha siku ya mtoto wa kike Duniani yenye kaulimbiu "Tokomeza Ndoa za Utotoni na Wekeza katika Haki za Wasichana." ambayo huadhimisha kila ifikapo tarehe 11 Oktoba, inayolenga kusisitiza ulinzi na haki za mtoto wa kike.

Kupitia taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari, TAMWA-ZNZ imesisitiza kuwa, ndoa za utotoni ni kikwazo kikubwa kwa maendeleoya mtoto wa kike, kwani zinaweza kumkatisha masomo, kuhatarisha afya yake, kumwathiri kisaikolojia na kumpunguzia fursa za kushiriki kikamilifu katika maendeleo yake na ya jajamii.

Aidha, TAMWA-ZNZ inakumbusha haki za mtoto wa kike zinalindwa na mifumo mbalimbali ya kisheria ya kitaifa na kimataifa, ikiwemo Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Mtoto (CRC), uliopitishwa tarehe 20 Novemba 1989 na kuanza kutumika tarehe 2 Septemba 1990. Mkataba huu unatambua haki za kila mtoto bila ubaguzi, ikiwemo haki ya kuishi, kukua, kupata elimu na huduma za afya, pamoja na kulindwa dhidi ya ukatili, unyonyaji na udhalilishaji.

Taarifa ya TAMWA-ZNZ inaeleza kuwa, Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto ((African Charter on the Rights and Welfare of the Child, 1990), kupitia Kifungu cha 16(1) na (2), unasisitiza wajibu wa kulinda watoto dhidi ya aina zote za ukatili, unyanyasaji na udhalilishaji, huku

Kifungu cha 21(1) na (2) kikitaka watoto walindwe dhidi ya mila na desturi zenye madhara, ikiwemo ndoa za utotoni, na kuweka umri wa chini wa ndoa kuwa miaka 18. Aidha, Kifungu cha 27(1) kinasisitiza ulinzi wa watoto dhidi ya unyonyaji na unyanyasaji wa kingono. Hivyo, Serikali, familia na jamii wana wajibu wa kuchukua hatua madhubuti za kuzuia ukatili wa kijinsia, kutokomeza ndoa za utotoni na kuhakikisha kila mtoto anakua katika mazingira salama yanayoheshimu haki, utu na ustawi wake.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.