Skip to main content

SIKU YA KUPINGA KUTOKUJALI UHALIFU DHIDI YA WANAHABARI: UKIWALINDA UMELINDA UKWELI

Leo, Novemba 3, jamii ya kimataifa inaadhimisha Siku ya Kupinga Kutokujali Uhalifu Dhidi ya Wanahabari.

SIKU YA KUPINGA KUTOKUJALI UHALIFU DHIDI YA WANAHABARI: UKIWALINDA UMELINDA UKWELI
Studio Narration JAMBO FM

SIKU YA KUPINGA KUTOKUJALI UHALIFU DHIDI YA WANAHABARI: UKIW...

0:00 --:--

Leo, Novemba 3, jamii ya kimataifa inaadhimisha Siku ya Kupinga Kutokujali Uhalifu Dhidi ya Wanahabari.

Siku hii ilitangazwa na Umoja wa Mataifa kupitia Baraza Kuu lake mwaka 2013.

Siku hii l, ilichaguliwa kwa kumbukumbu ya tukio la kusikitisha la Novemba 2, 2013, nchini Mali, ambapo wanahabari wawili walipoteza maisha wakiwa katika kazi yao ya kutafuta taarifa.

Tangu hapo, Umoja wa Mataifa umekuwa ukitumia siku hii kuhamasisha ulimwengu kuhusu umuhimu wa kulinda wanahabari.

Kauli Mbiu ya 2026:

Mwaka huu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) linaongoza maadhimisho haya kwa kauli mbiu isemayo:

Kulinda Wanahabari ni Kulinda Ukweli:

Ujumbe huu unasisitiza kuwa kazi ya mwanahabari ni muhimu kwa kila jamii.

Kwa Nini Siku Hii ni Muhimu?

Wataalamu wa habari na maendeleo wanaeleza kuwa uhuru wa kupata habari una faida kubwa kwa kila mtu:

1. Kwa Elimu: Habari sahihi huwasaidia wanafunzi na wazazi kujua fursa za masomo.

2. Kwa Afya: Habari za afya huwasaidia wananchi kujua jinsi ya kujikinga na magonjwa.

3. Kwa Maendeleo: Habari kuhusu kilimo, biashara na teknolojia huwasaidia wananchi kujiletea maendeleo.

4. Kwa Amani: Taarifa sahihi hupunguza uvumi na kusaidia kudumisha amani katika jamii.

Shirika la UNESCO linasema kuwa jamii inapopata taarifa sahihi na kwa wakati, wananchi wake wanaweza kufanya maamuzi bora ya kimaisha.

Takwimu za Ulimwengu:

Kwa mujibu wa UNESCO, katika miaka kumi iliyopita, kumekuwa na jitihada kubwa duniani za kuongeza usalama wa wanahabari. Mashirika mbalimbali yamekuwa yakitoa mafunzo ya usalama kazini na namna ya kuepuka vitisho vya kidijitali.

UNESCO pia inaeleza kuwa, waandishi wa habari na wafanyakazi wa vyombo vya habari 189 waliuawa kati yam waka 2024 na 2025, takwimu hizi zikionesha uhalisia kuwa,kuripoti ukweli bado kunawagharimu waandishi wa habari maisha yao, huku haki ikiendelea kuwa kitu kigumu kupatikana kwa waathiriwa wengi na familia zao.

Kwenye eneo la Afrika Mashariki na Maziwa Makuu, tathmini ya shirika la Wanahabari Wasio na Mipaka, RSF, inazitaja nchi za Tanzania, Rwanda, DRC, Uganda, Burundi na Kenya.

Hizo ni miongoni mwa nchi ambazo waandishi wa habari wanakabiliwa na changamoto kubwa kuanzia mashambulizi ya kimwili, kukamatwa kiholela, hadi sheria kandamizi za vyombo vya habari na shinikizo la kiuchumi.

Barani Afrika, Taasisi ya Kimataifa ya Vyombo vya Habari, ilirekodi matukio 100 ya vitisho na mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari katika nchi 22 zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara kati ya Aprili na Juni 2026,

Mashambulizi ya kimwili, kukamatwa na kuwekwa kizuizini, vilikuwa miongoni mwa ukiukwaji ulioripotiwa mara nyingi zaidi, huku polisi na vyombo vya usalama vya serikali vikihusika na asilimia 55 ya lmatukio haya.

Maadhimisho ya siku hii hufanyika kwa njia mbalimbali duniani, ikiwemo semina za kitaaluma, mijadala ya wanafunzi wa vyuo vya habari, na makongamano ya kubadilishana uzoefu.

Hitimisho:

Siku ya Kupinga Kutokujali Uhalifu Dhidi ya Wanahabari ni nafasi ya kutafakari mchango wa taarifa sahihi katika kujenga jamii yenye uelewa na maendeleo. Ni siku ya kuthamini umuhimu wa ukweli na taarifa sahihi katika maisha ya kila siku.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.