Na Cecilia Shiratu - Kagera.
Meneja wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) mkoa wa Kagera, Mhandisi Peter Kilima ameeleza kuwa, vijana 90 wamepata mafunzo ya ujasirimali, wenye umri Kati ya miaka 15 hadi 45 yanayolenga kuwapatia vijana ujuzi katika fani ya usindikaji wa vyakula, sabuni, ususi, urembo na ushonaji.
Vijana hao ni miongoni mwa wananchi walioguswa na Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), wamepatiwa mafunzo ya wiki moja na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo Tanzania (SIDO), pamoja na Shirika lisilo la kiserikali la Sheria Kiganjani Mkoa wa Kagera.

Aidha, Mkurugenzi wa mafunzo na usimamizi wa mikoa wa SIDO Tanzania, George Kasinga, ameeleza kuwa mafunzo hayo yamelenga zaidi kuwawezesha vijana na kinamama kutumia vizuri ujuzi na fursa zilizopo katika jamii kujiajiri na kuendesha maisha yao.
Naye, Mkufunzi wa fani ya utengenezaji na uzalishaji wa sabuni SIDO,Beatus Pancras ameiomba serikali kuwapatia wawekezaji na wadhabuni watakao wasaidi kuongeza upatikanaji wa malighafi hasa mafuta ya mawese na vifaa vya kutengenezea sabuni (molding) ambavyo vitarahisisha na kusaidia vijana kujikwamua kiuchumi.

Pancras ametoa wito kwa vijana kutokaa mtaani amewaomba waje SIDO kupata mafunzo na ujuzi katika fani mbalimbali yanakayowawezesha kutimiza ndoto zao.
Nao baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo wamesema, SIDO imekuwa mwanga wa mafanikio kwao Kwani ujuzi walopata utawawezesha vijana hao kujiari katika biashara ndogo, kuongeza kipato na pia kuajiri vijana wengne.
Discussion
Reader comments
0 contributions