Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga limeombwa kupeleka nishati ya umeme katika shule ya Msingi Mlimani na Mtakuja ambazo tayari zimefungwa miundombinu ya umeme zilizoopo katika kata ya Nyahanga manispaa ya Kahama.
Akizungumza katika baraza la madiwani la Manispaa ya Kahama katika kikoa cha kawaida, diwani wa kata ya Nyahanga Josephina Kilimba ametaka kujua ni lini shule hizo zitapelekewa nishati ya umeme ili kuweza kurahishisha kazi katika shule hizo.

“Mhe mwenyekiti mi nina swali kuhusu suala la umeme katika shule ya msingi Mlimani na Mtakuja,shule hizi tayari zimeshafungiwa miundombinu yote ya Umeme ila hadi sasa umeme bado haujafika shuleni sasa ni lini umeme utafika katika shule hizi,” amesema Kilimba.
Aidha, Kilimba amesema kuwa kuna baadhi ya taasisi zikiwemo shule, zahanati na vituo vya afya katika maeneo mengine hazijafikiwa kupata nishati hiyo na kuomba serikali kushughulikia changamoto hiyo.

“Lakini Mh.Mwenyekiti si shule hizi tu,bali kuna taasisi zingie za serikali hazijafikiwa na huduma ya nishati ya umeme zikiwemo zahanati na vituo vya afya,sasa tuiombe serikali itusaidie kufikisha huduma hii muhimu ili iwe rahisi katika kuwahudumia wananchi,” aliongeza Kilimba.
Kwa upande wake, Mhandisi kutoka TANESCO wilaya ya Kahama, Ones Mbembe akijibu swali hilo amesema kuwa ndani ya mwaka wa fedha ujao katika maeneo ya taasisi ambayo hayajafikiwa na umeme yatafikiwa, huku kwa sasa wakifanyia kazi na watendaji wa kata katika kuainisha maeneo hayo.

“Mh Mwenyekiti ni kweli maeneo mengi ya ofisi ya serikali huduma ya umeme haijafika,ila katika mwaka wa fedha ujao maeneo yote ya taasisi za umma ambazo hayajafikiwa na huduma ya umeme yatapata umeme,” amesema Mbembe.
Naye, mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama Thomas Myonga, mewapongeza na kuwataka madiwani wa Mnispaa ya Kahama kuendelea kuwatumikia wananchi kwa kusikiliza na kutatua kero zao.
“Niwapongeze sana waheshimiwa madiwani kwa juhudi zenu kubwa za kuzifikisha kero za wananchi kwa ajili ya kupatiwa utatuzi,niwaombe sana endeleeni kuwatumia wananchi kwa kusikiliza kero zao na kuzitatua,” alisema.
Discussion
Reader comments
0 contributions