Skip to main content

SHUGHULI ZASIMAMA KAHAMA MADEREVA BAJAJI WAKIUAGA MWILI WA MWENZAO

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

SHUGHULI ZASIMAMA KAHAMA MADEREVA BAJAJI WAKIUAGA MWILI WA MWENZAO

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

Umoja wa madereva wa pikipiki za magurudumu matatu manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga leo asubuhi ya June 16 wamesitisha shughuli zao za usafirishaji kwa lengo la kumuaga dereva mwenzao aliyefariki June 14 kwa kugongwa na gari.

Tukio hilo liliwalazimu baadhi ya abiria wanaotumia usafiri huo kushushwa kwenye bajaji wakiendelea na safari kisha madereva hao kujiunga kwenye mstari ili kusubiri msafara wa kumsindikiza mwenzao kuelekea kishapu kwa ajili ya mazishi.

Wakizungumza na Jambo Fm baadhi ya wananchi wamesema kuwa madereva hao wangekuwa wastaarabu na kuacha kuziba barabara na kutoa ushauri waombe kibari kwa jeshi la polisi pindi wanapotaka kufanya mikusanyiko ambayo inazuia shughuli zingine kuendelea.

“Nimeshangaa sana leo abiria wanashushwa na bajaji haziendi popote,sasa hali hii inaleta sintofahamu kwa wananchi mana njia zimeziba hapa katikatikati yam ji,Tunajua ndiyo wana umoja wao lakini wanapotaka kufanya hivi wachukue kibali cha usalama barabarani maana inakuwa kero kwa wananchi” Wamesema baadhi ya wananchi hao.

Sambamba na hayo wananchi hao wameliomba jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kutenga njia maalumu ya kupita kwa watu wanaokuwa wengi wanaotaka kufikisha ujumbe wao kwa jamii au serikali.

“Hatukatai wana umoja kuandamana bali wasiandamane kila sehemu,tuliombe jeshi  la polisi kitengo cha usalama barabarani wawatengee barabara maalum kwa ajili ya kupita ila wasiwabugudhi wananchi na shughuli zao za kiuchumi” Ameongeza Mzee Saidi Damasi mkazi wa mtaa wa Lumelezi.

Naye mwenyekiti wa umoja wa madereva pikipiki za biashara za matairi mawili na matatu mkoa wa Shinyanga Idsam Mapande amesema kuwa msululu wa madereva hao ni jambo la kawaida katika umoja wao kwani mara kwa mara wamekuwa wakijikusanya kwa ajili ya kuaga mwili wa dereva mwenzao aliyefariki na kwamba hali hiyo ni desturi na taratibu za umoja wao.

“Leo tupo hapa kwa ajili ya kumuaga mwenzetu ambaye alipata ajali siku ya tarehe 14 June na leo tunamuaga hapa kwa ajili ya safari ya kuelekea Kishapu, huu ni utaratibu wetu,"

"sema kwakuwa maafisa usafirishaji tuko wengi na watu hawajazoe kutuona kwa Pamoja ndo mana wanasema tumefunga barabara, siyo kweli sisi tunamuaga mwenzetu na jeshi la polisi liko hapa kuhakikisha magari yote yanapita kwa usalama bila shija,” amesema Mapande.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Usalama barabarani manispaa ya Kahama Mrakibu wa polisi Frorah Nangawe amesema kuwa walikuwepo eneo la  tukio katika kuhakikisha barabara zote zinapitika bila shida na kwamba hakuna tukio lolote la uvunjifu wa amani lilijitokeza wakati madereva hao wakimuaga mwenzao.

“Sisi tulikuwepo eneo la tukio na tumehakikisha kuwa barabara zote zinapitika muda wote lengo ni kwamba shughuli yao ya kuaga mwili wa ndugu yao iendelee na shughuli zingine za matumizi ya barabara zifanyike” Amesema Nangawe.

Nao baadhi ya madereva bajaji manispaa ya Kahama wamesema kuwa wamepokea kwa masikitiko kifo cha dereva mwenzao kilichotokea kwa uzembe wa dereva wa gari kubwa na kuwaomba madereva wa magari kuheshimu sheria za barabarani na kuheshiana mwenye chombo kikubwa na kidogo.

“Huu msiba umetuuma sana niwaombe madereva wenzetu wa magari tuzingatie sheria na tuheshiane barabarani kwani sote sisi ni madereva bila kujalisha ukubwa wa chombo unachoendesha.” Wamesema madereva hao.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.