Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita leo Oktoba 7, 2026 amefanya ziara katika kitongoji cha Shialabela kilichopo katika kijiji Ng'wang'alanga kata ya Samuye Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, ili kuzungumza na wakazi wa eneo hilo juu ya tahadhari za kuchukua katika mkondo wa maji kuelekea mto Manonga.

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA MBONI MHITA
Amesema, mwaka 2024 kulitokea mafuriko katika katika eneo hilo na ilisababisha adha kubwa kwa wakazi wa eneo hilo kwakuwa mahali hapo ni mkondo wa maji hivyo amewataka wakazi wa eno hilo kuondoka mara moja na kuelekea maeneo salama mvua zitakapoanza pindi wakiona athari zinaanza kujitokeza ili zisilete madhara.
RC Mboni amesema kama mvua zitanyesha juu ya wastani kama ambavyo inatabiliwa na mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) basi mvua hizo zitakuwa ni kubwa sana katika hali ambayo haielezeki, na ukweli usiofichika ni kwamba wakazi hao wanaishi kwenye mapito ya maji ambayo yanapitisha maji kwenda mto Manonga hivyo wakazi hao wanapaswa kutambua kuwa wapo katika maeneo hatarishi.
"Ni sawa ni kitongoji tumejenga lakini ni lazima tuendelee kukumbushana kuhusina na tahadhari kwani eneo hilo ni bonde na mvua zitakapoanza kunyesha tutakutana na changamoto kubwa na sisi kama serikali hatuko tayari changamoto hiyo itokee"amesema RC Mboni

Amesema serikali kupitia halimashauri ya wilaya ya Shinyanga tayari imeanisha maeneo salama ya kuelekea pindi mvua hizo zitakapoleta madhara na kuwataka wananchi hao wasingojee mvua izidi ndio waelekee kwenye maeneo hayo kwa ni serikali haitaki kupata watu amabo ni majeruhi kwa kuangukiwa na matofali au kupata chngamoto mbalimbali za afya au vifo hivyo tahadhari kabla ya hatari ni jambo la msingi.

Akizungumzia eneo hilo mkurugenzi mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Shinyanga Dr Kalekwa Kasanga amesema halimashauri yake imeshaanisha maeneo ambayo ni hatarishi katika mvua hizo likiwemo eneo hilo, lakini pia imeainisha maeneo ambayo ni salama pindi athari zikianza kujitokeza likiwemo eneo la shule ya msingi Kabale.
MKURUGENZI MTENDAJI HALIMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA DR KALEKWA KASANGA
Dedan Makungu ni mkazi wa kijiji hicho cha Ng'wamang'alanga ambapo anakiri kuwa kijiji hicho kimekuwa kikijaa maji katika nyakati za mvua mpaka kuangusha majengo kwa sababu njia yake imezibwa kwani kumekuwa na majaruba mengi ya mpunga yametengenezwa katika eneo hilo ambapo awali palikuwa ni njia ya maji na kuitaka serikali kusaidia kuzibuz majaruba hayo ili kijiji hicho kisiendelee kusumbuliwa na maji.

DEDAN MAKUNGU MKAZI WA KIJIJI CHA NGW'AMANG'ALANGA
Naye John Joseph ambaye ni mkazi wa kijiji ameiomba serikali kufanya ukarabati wa barabara katika eneo la kona upande wa mashariki katika barabara kuu ya kijiji hicho na kuwekwa kalavati ili maji yawe yanapita kwa urahisi na kuepuka kuleta madhara.
JOHN JOSEPH MKAZI WA KIJIJI CHA NGW'AMANG'ALANGA

VIONGOZI KATIKA MKOA WA SHINYANGA WAKIFANYA UKAGUZI KATIKA MKONDO WA MAJI MTO MANONGA

BAADHI YA WANANCHI WALIOJITOKEZA KUMSIKILIZA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA MBONI MHITA
JESHI LA SUNGUSUNGU KATIKA KIJIJI CHA NG'WAMANG'ALANGA WAKIMSIKILIZA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA MBONI MHITA
Discussion
Reader comments
0 contributions