Na Eunice Kanumba – Shinyanga.
Mkoa wa Shinyanga, unatarajiwa kuwa mwenyeji wa maonesho ya tano ya kitaifa ya bidhaa yanayoratibiwa na shirika la maendeleo la viwanda vidogo (SIDO) yanayotarajia kuanza Oktoba 21-30, 2026, lengo likiwa ni kuwaleta wajasiliamali pamoja ikiwa ni pamoja na kubadilishana ujuzi, ubunifu na uzoefu miongoni mwao na kuongeza uzalishaji utakaowapelekea kuinuka kiuchumi.
Akizumgumza na waandishi wa habari mkoani Shinyanga kuhusiana na maonesho hayo, Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Tanzania, Mhandisi Syilivesta Mpanduji amesema, maonyesho hayo yatawakusanya Zaidi ya wajasiliamali 600 kutoka Tanzania bara na visiwani,pamoja na taasisi za serikali na zisizokuwa za serikali Zaidi ya 50, na kwamba maonyesho hayo yatafanyika katika uwanja wa Magufuli katika manispaa ya Kahama mkoani humo.
Amesema , kupitia maonyesho hayo wajasiriamli watapata fursa ya kujifunza na kuongeza wigo wa kuuza na kutambulisha bidhaa wanazozalisha ikiwa ni pamoja na kutoa fursa ya kuonyesha teknolojia mbalimbali zinazotoa fursa ya kuzalisha bidhaa hapa nchini.

Aidha, Mhandisi Mpandiji ameongeza kuwa katika upendeleo wa pekee kundi la vijana litapewa fursa ya kuonyesha bidhaa mbalimbali wanazolisha katika miradi wanayoitekeleza lengo likiwa ni kuongeza wigo wa bidhaa za soko la kati kwa vijana kote nchini
Kwa upande wake kaimu katibu tawala mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi amesema maonesho hayo maonesho hayo kwa mwaka huu yamefanyika katika eneo sahihi, kwani Manispaa ya Kahama ni mji unaokuwa kwa kasi lakini pia ni kitovu cha biashara na wajasiliamali.
Lyamongi amesema mkoa wa Shinyanga upo tayari kwa maonyesho hayo huku akiwataka wadau wote kushiriki mashindano hayo na kuwataka wajasiliamali wote katika mkoa wa Shinyanga kutumia fursa hiyo kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maonyesho hayo
Amezitaka sekta binafsi na mkampuni makubwa pamoja na taasisi za kifedha yakiwemo mabenki katika mkoa huo kuijitokeza kudhamini maonyesho hayo ili yafanyike kwa weledi na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi yakiwemo maakundi maalumuya vijana na wanawake kujitokeza kujifunza namana ya kuanzisha viwanda vidogo
Nao baadhi ya wadau waliojitokeza katika kikao hicho cha waandishi wa habari akiwemo Kaimu meneja wa SIDO mkoa wa Shinyanga, Ally Mtware amewaomba Wajasirimali wote kujitokeza kwa wingi waweze kutafuta masoko huku mhahiri msaidizi wa chuo kikuu cha ushirika Moshi tawi la Kizumbi manispaa ya Shinyanga John Mwera akiwataka vijana kujitokeza kwa wingi ili kujifunza ushindani katika teknolojia.
Discussion
Reader comments
0 contributions