Skip to main content

SHERIA, KANUNI ZA UTUMISHI WA UMMA ZIZINGATIWE KUBORESHA UTENDAJI - DKT. FATMA

Na Saulo Stephen - Singida.

SHERIA, KANUNI ZA UTUMISHI WA UMMA ZIZINGATIWE KUBORESHA UTENDAJI - DKT. FATMA

Na Saulo Stephen - Singida.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Fatuma Mganga amewataka Viongozi na watumishi wa Umma kutumia elimu waliyoipata katika mafunzo ya uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia utumishi wa umma, ili kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa taasisi za Umma, Dkt. Mganga amesema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa wa watumishi wa umma kuhusu sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uwajibikaji na kwa kuzingatia misingi ya utawala bora.

Ameongeza kuwa, Serikalini inaendelea kuboresha mazingira ya kazi na maslahi ya watumishi wa umma, hivyo ni wajibu wa watumishi hao kutekeleza majukumu yao kwa bidii, uaminifu na kuzingatia maadili ya kazi pamoja na sheria na taratibu zilizowekwa.

Aidha, amesema kupitia mafunzo hayo, watumishi wa umma wataweza kupata uelewa mpana wa namna bora ya kushughulikia masuala ya kiutumishi na kinidhamu, jambo litakalosaidia kupunguza malalamiko na rufaa zisizo za lazima pamoja na kuongeza uwajibikaji na ufanisi katika utendaji kazi.

Hata hivyo, amewataka washiriki kutumia maarifa waliyoyapata katika maeneo yao ya kazi ili kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kuchangia maendeleo ya taasisi zao pamoja na Taifa kwa ujumla.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.