Skip to main content

SHEREHE ZA UKOSEFU WA MAADILI: NANI ANATOA VIBALI? - WAITARA

Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara amehoji iwapo Serikali ilitoa kibali cha kufanyika kwa sherehe zinazohusishwa na vitendo vya usagaji jijini Dar es Salaam.

SHEREHE ZA UKOSEFU WA MAADILI: NANI ANATOA VIBALI? - WAITARA
Studio Narration JAMBO FM

SHEREHE ZA UKOSEFU WA MAADILI: NANI ANATOA VIBALI? - WAITARA

0:00 --:--

Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara amehoji iwapo Serikali ilitoa kibali cha kufanyika kwa sherehe zinazohusishwa na vitendo vya usagaji jijini Dar es Salaam.

Waitara ameuliza swali hilo Bungeni jijini Dodoma, kutokana tukio hilo kuonekana katika mitandao mbalimbali ya kijamii na kuzua gumzo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Eng. Maryprisca Mahundi, amesema Serikali haiungi mkono wala kuzipa uhalali.

Amesema, Serikali itaendelea kusimamia sheria na miongozo ya nchi, huku akizitaka familia na jamii kuimarisha malezi ya watoto kwa kuzingatia mila, desturi na maadili.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.