Skip to main content

SHEIKH SIMBA AWAHIMIZA WAFANYABIASHARA WA NYAMA SINGIDA KUSITISHA MGOMO

Na Saulo Stephen - Singida.

SHEIKH SIMBA AWAHIMIZA WAFANYABIASHARA WA NYAMA SINGIDA KUSITISHA MGOMO
Studio Narration JAMBO FM

SHEIKH SIMBA AWAHIMIZA WAFANYABIASHARA WA NYAMA SINGIDA KUSI...

0:00 --:--

Na Saulo Stephen - Singida.

Baada ya mgomo wa Wafanyabiashara wa Nyama mkoani Singida, Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Singida, Sheikh Issa Simba, amewataka kuendelea na biashara hiyo, akisisitiza kuwa huduma ya nyama ni muhimu kwa wananchi.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake leo, Sheikh Simba amesema Serikali imekuwa ikiweka mipango mbalimbali kwa lengo la kuleta maendeleo na kuboresha maisha ya wananchi, hivyo ni muhimu wafanyabiashara kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa mipango hiyo.

Amesema wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla wanapaswa kufuata maelekezo yanayotolewa na viongozi wa Serikali ili kuhakikisha amani, utulivu na mshikamano vinaendelea kudumishwa.

Sheikh Simba amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya Serikali, wafanyabiashara na wananchi ni muhimu katika kutatua changamoto zinazojitokeza, huku akiwataka wafanyabiashara wa nyama kurejea katika shughuli zao na kuhakikisha huduma hiyo muhimu inaendelea kupatikana kwa wakazi wa Manispaa ya Singida.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.