Skip to main content

SHEIKH RAJAB ASISITIZA UTIIFU, HESHIMA KWA MAMLAKA

Na Gideon Gregory - Dodoma.

SHEIKH RAJAB ASISITIZA UTIIFU, HESHIMA KWA MAMLAKA

Na Gideon Gregory - Dodoma.

Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu Shaaban amesema waumini wa dini ya Kiislamu wanapaswa kuendeleza usikivu, utiifu na kuheshimu mamlaka ili kudumisha amani na mshikamano katika jamii na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza katika ibada ya Eid El Hajj iliyofanyika leo Mei 27,2026  katika Msikiti wa Gaddafi, Jijini Dodoma,Sheikhe Shaaban amesema makumi ya mwezi wa Dhulhijjah yamehitimishwa leo huku akiwaasa Waislamu wenye uwezo kutekeleza ibada ya kuchinja kama ilivyoelekezwa katika dini ya Kiislamu.

Amesema  ibada hiyo ni tukio la kihistoria lililoanzia kwa Nabii Ibrahim na mwanawe Nabii Ismail, ambapo waumini wanajifunza usikivu, utiifu na kuheshimu maagizo ya Mwenyezi Mungu.

“Si hadithi ya kawaida, ni simulizi inayotufundisha utiifu na usikivu. Nabii Ibrahim alimweleza mwanawe kuwa ameona katika ndoto anamchinja, jambo linalotufundisha namna ya kuheshimiana, kusikilizana na kutii mamlaka,” amesema.

Amesema jamii inapokosa usikivu na utiifu ndipo migogoro na umwagaji damu hujitokeza, hivyo wananchi wanapaswa kuendelea kuishi kwa amani, kuheshimiana na kusikilizana ndani ya familia na katika Taifa.

Aidha, amesisitiza kuwa dini inaelekeza waumini kuwatii Mwenyezi Mungu, Mtume Muhammad pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, dini na kisiasa.

Sheikhe Shaaban pia amewataka wananchi kuheshimu taasisi na vyombo vinavyoundwa kwa ajili ya kusimamia masuala mbalimbali ya jamii na dini, akitolea mfano tume na kamati zinazoundwa ndani ya taasisi za kidini kama BAKWATA.

Amesema ni muhimu kwa jamii kujenga utamaduni wa kuheshimu maamuzi ya viongozi na taasisi halali ili Taifa liendelee kuwa na utulivu, mshikamano na maendeleo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.