Skip to main content

SHANWE: BOX KALVATI YAFUNGUA NJIA MPYA KWA WANANCHI

Fursa za usafiri, biashara na mawasiliano zimeanza kufunguka kwa wananchi wa Kata ya Shanwe, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Box Kalvati katika barabara ya Mikocheni JCT–White Giraffe, kupitia Mpango wa Tanzania Cities Transforming Infrastructure and Competitiveness — TACTIC.

SHANWE: BOX KALVATI YAFUNGUA NJIA MPYA KWA WANANCHI
Studio Narration JAMBO FM

SHANWE: BOX KALVATI YAFUNGUA NJIA MPYA KWA WANANCHI

0:00 --:--

Fursa za usafiri, biashara na mawasiliano zimeanza kufunguka kwa wananchi wa Kata ya Shanwe, Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Box Kalvati katika barabara ya Mikocheni JCT–White Giraffe, kupitia Mpango wa Tanzania Cities Transforming Infrastructure and Competitiveness — TACTIC.

Kwa muda mrefu, mto uliopo katika eneo hilo ulikuwa kikwazo cha shughuli za wananchi, hasa wakati wa mvua, huku wanafunzi nao wakikumbana na changamoto wakati wa kwenda na kurudi shuleni.

Hata hivyo, kukamilika kwa Box Kalvati hiyo sasa kumebadilisha hali, kwa kuwa wananchi wamepata njia salama na rahisi zaidi ya kuvuka eneo hilo, jambo linalotarajiwa kuongeza ufanisi wa shughuli zao za kila siku.

Daines Lumbwe, mkazi wa Kata ya Shanwe, amesema kukamilika kwa Box Kalvati hiyo kumewaondolea wananchi hofu na usumbufu waliokuwa wakikabiliana nao, hususani kipindi cha mvua.

“Awali tulikuwa tunapata shida sana kuvuka hapa, hasa wakati wa mvua. Watoto wa shule nao walikuwa wanapata changamoto wanapokwenda na kurudi shule, lakini sasa hali imekuwa tofauti,” amesema Lumbwe.

Mbali na usalama wa watumiaji wa barabara, Box Kalvati hiyo inatarajiwa kufungua zaidi mawasiliano kati ya Kata za Makanyagio, Shanwe na Kasokola, pamoja na kurahisisha usafirishaji wa wananchi wanaofika katika soko la matunda.

Mradi huo ni sehemu ya uwekezaji mkubwa wa TACTIC wenye thamani ya Shilingi bilioni 21.9, unaohusisha ujenzi wa kilomita 8.49 za barabara kwa kiwango cha lami, ufungaji wa taa 400 za barabarani pamoja na ujenzi wa jengo la kudumu la ofisi za wahandisi wasimamizi wa miradi.

Ujenzi wa Box Kalvati hiyo pekee umegharimu zaidi ya Shilingi milioni 349.7 na umefikia asilimia 100 ya utekelezaji, wakati mradi mzima ukiwa umefikia asilimia 40.

Hata hivyo, matumizi yake kwa kiwango kamili yataanza baada ya kukamilika kwa matabaka ya lami yanayofuata katika barabara hiyo.

Akizindua Box Kalvati hiyo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Wazo Michael Mwang’onda, amewataka wananchi kulinda miundombinu hiyo na kuendelea kudumisha amani ili kuwezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye kugusa maisha ya wananchi moja kwa moja.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.