Jina lake ni Shaka Senzangakhona marufu kama 'Shaka Zulu', mzaliwa wa mwaka 1787 huko Kwazulu-Natal Afrika Kusini, ambaye aliishi hadi mwaka 1828 alipofariki akiwa na miaka 41.
Alikua Mfalme wa Himaya ya Wazulu huko Afrika Kusini kuanzia mwaka 1816 –1828 alkirithi Ufalme kutoka kwa Baba yake Senzangakhona kajama.
Jina la shaka ali0ewa kutokana na neno la kizulu "iShaka" linalomtaja mdudu ambaye katika imani ya Utamaduni wa Kizulu, akisemekana kuvuruga Hedhi ya wakinamama na alipewa jina hilo kwa kuwa alizaliwa nje ya utaratibu.
Sifa zake zimetokana na uwezo wa kupanua utawala wake kutoka eneo ndogo la 260 km² kuwa 28,500 km², kuvunja nguvu ya makabila mengine na kuyaunganisha na taifa lake.

Katika historia ya Kijeshi ya Afrika alianzisha mbinu mpya zilizopanua uwezo na enzi yake.
Shaka Zulu alimpenda Sana Mama yake Mzazi 'Nandi kaBhebhe' kiasi kwamba Mama yake huyo alipofariki October 10, 1827, Shaka akaanza kufanya mauaji.
Zaidi ya watu 7,000 waliuawa na Shaka Zulu ndani ya Mwaka mmoja tu.
Pia, alipiga Marufuku mtu yeyote wa Wazulu kupanda zao lolote shambani kwa mwaka huo.

Katika moja ya visa vilivyobaki kuwa kumbukumbu ya ujasiri, ni pale ambapo Shaka Zulu alipopewa amri na wakoloni kwamba aachane na Mila/Tamaduni na aipokee Dini vinginevyo atachomwa moto akiwa hai, lakini akawajibu kwamba "Huku kwetu tunakula moto"
Mengi yakasemwa kumuhusu lakini Dokta Maxwell Zakhele Shamase akaamua kutenganisha ukweli na uongo, akishirikiana na Mthandeni Patrick Mbatha, mwanahistoria kutoka Chuo Kikuu cha Zululand kwa kuamua kuandika kitabu kuhusu maisha ya Shaka Zulu.
Wanasema, kabla ya kuzaliwa kwa Shaka, nabii kwa jina la Sithayi, alibashiri kwamba 'kutazaliwa mtoto ambaye ataleta mfumo mpya wa utawala na kuanzisha taifa jipya.'
Na ndiyo maana alikuwa ni mjuzi wa mikakati ya vita barani Afrika, alikuwa ni mjenzi wa taifa na sio kiongozi anaependa kumwaga damu kwani hakuwa muuwaji asiye na huruma.

Kama kamanda, aliwalazimisha mashujaa wake kutovaa viatu na kutembea pekupeku, akizuia pia matumizi ya mikuki mirefu ambayo mashujaa wake waliitumia dhidi ya maadui wao.
Aliwataka watumie mikuki mifupi kwa mapambano ya karibu zaidi, mkakati ambao uliwalazimisha wapiganaji wake kutumia mkuki mmoja kupigana na maadui wengi zaidi.
Pia alianzisha mkakati wa kuwazunguka wapinzani wao kabla ya kuwavamia, maarufu kama "pembe za nyati." Shaka Zulu alikuja kuwa mtu anaeogopwa sana na kupata umaarufu hata kwenye makabila na falme nyinginezo.
Hili lilisababisha kipewa jina la 'Nodumehleli' likiwa na maana ya ambaye akiketi ardhi hutikisika.
Baba yake Senzangakhona alipofariki, Mfalme Dingiswayo alimsaidia kurudi kwa watu wa baba yake, na kumpa mashujaa wawili kuongozana naye kumsaidia kukamata madaraka.

Lakini Mfalme Senzangakhona alimwambia waziri mkuu wake Mudli, kwamba mtoto mwengine wa kiume Sigujana ndiye atakaerithi kiti cha ufalme, na sio Shaka.
Hapo ndipo Shaka alipomuuwa Sigujana na mwaka 1816 alijitangaza Mfalme na baada ya Mfalme Dingiswayo kufariki, Shaka aliwajumuisha watu wa Mthethwa chini ya ufalme wake.
Shaka hakuunga mkono suala la ndoa kutokana na alivyoshuhudia yaliyomkuta mama yake.
Na utotoni mwake mara nyingi alikuwa akifanyiwa utani kwa vile hakulelewa na baba yake, alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanawake tofauti, lakini pindi wakishika mimba alikuwa alimtunukia ndugu yake wa kiume ambaye alikuwa akionekana kama mtu dhaifu.
Aliuliwa mnamo mwaka 1828 baada ya uwepo wa njama iliyopangwa na shangazi yake. Sababu kuu ni kwamba baada ya kifo cha mama yake Shaka alirukwa na akili na akawa anaua watu bila ya kufikiria mara mbili kwa kisingizio cha kuwa na huzuni ya kufiwa na mzazi wake.
Baadhi aliwaua kwa kumfanyia utani utotoni mwake, na wengine aliwaua kwa kutoonyesha huzuni vya kutosha wakati wa kifo cha mama yake.
Shaka Zulu alikuwa ni mbabe wa kivita na sio Napoleon mweusi. Kwanini usiseme Napoleon alikuwa Shaka mweupe?
Hii ni kwasababu hakuwahi kwenda Ulaya, na hakuna mzungu aliyemfunza mikakati aliyoitumia wakati wa vita, bali yote ilikuwa ni mipango yake mwenyewe.
Visa vyake vinagusia muunganiko yaani namna alivyowaunganisha watu wa Zulu, kwa mfano Chama cha Inkatha Freedom kinachoongoza katika jimbo la Kwazulu Natal kinamtambua Mfalme Shaka.
Aidha, Wafalme wa Zulu pamoja na watu wao bado wanamuenzi Mfalme Zulu hadi hii leo.
Discussion
Reader comments
0 contributions