Skip to main content

SERIKALI:VYUO VIKUU GEUZENI TAFITI NA MAARIFA KUWA SULUHU YA CHANGAMOTO ZA JAMII

Serikali imesisitiza Vyuo Vikuu na Taasisi za utafiti kubadili maarifa na tafiti kuwa suluhisho za changamoto za jamii kwa kuimarisha tafiti shirikishi zinazowakutanisha watafiti, watunga sera, sekta binafsi na jamii.

SERIKALI:VYUO VIKUU GEUZENI TAFITI NA MAARIFA KUWA SULUHU YA CHANGAMOTO ZA JAMII
Studio Narration JAMBO FM

SERIKALI:VYUO VIKUU GEUZENI TAFITI NA MAARIFA KUWA SULUHU YA...

0:00 --:--

Serikali imesisitiza Vyuo Vikuu na Taasisi za utafiti kubadili maarifa na tafiti kuwa suluhisho za changamoto za jamii kwa kuimarisha tafiti shirikishi zinazowakutanisha watafiti, watunga sera, sekta binafsi na jamii.

Wito huo umetolewa leo Septemba 23, 2026 jijini Arusha na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir wakati akifungua Mkutano wa Tatu wa Muungano wa Vyuo Vikuu Vitano unaojumuisha Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST), Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Aga Khan na Chuo Kikuu cha Simon Fraser cha nchini Canada.

Amehimiza Vyuo hivyo kutumia uwezo wao wa pamoja katika utaalamu, miundombinu, tafiti na ubunifu, na kujenga miradi ya pamoja yenye malengo na matokeo yanayopimika.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) Prof. Maulilio Kipanyula ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuweka msisitizo na kutoa kipaumbele katika elimu, sayansi, teknolojia, utafiti na ubunifu, ikitambua kama nguzo muhimu za kuchochea maendeleo endelevu na kutatua changamoto za jamii.

Amesema kuwa NM-AIST inalenga kuwawezesha wanafunzi na watafiti kuzalisha maarifa, kuendeleza teknolojia na kubuni suluhisho zinazoweza kutumika katika jamii na viwanda, sambamba na kujenga uwezo wa ujasiriamali kwa ajili ya maendeleo.

Balozi wa Canada nchini Tanzania Emily Burns, ameupongeza Muungano wa Vyuo hivyo kwa kuendeleza ushirikiano wa Kimataifa, utafiti na ubunifu, akisisitiza kuwa Canada itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza maendeleo shirikishi na endelevu.

Amesema Serikali ya nchi hiyo, kupitia Chuo Kikuu cha Simon Fraser imeunga mkono Kituo cha Canada cha Ubunifu na Mabadilishano ya Maarifa, kitakachoonesha bunifu katika akili undea mabadiliko ya tabianchi na kilimo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.