Skip to main content

SERIKALI YAWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAFANYABIASHARA KIGOMA

Wizara ya Viwanda na Biashara imesema itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi wenye nia ya kuanzisha na kuendeleza biashara mkoani Kigoma, huku ikiwataka wafanyabiashara kutumia maonesho ya biashara kama fursa ya kutangaza na kukuza shughuli zao.

SERIKALI YAWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAFANYABIASHARA KIGOMA
Studio Narration JAMBO FM

SERIKALI YAWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAFANYABIASHARA KIGOMA

0:00 --:--

Wizara ya Viwanda na Biashara imesema itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi wenye nia ya kuanzisha na kuendeleza biashara mkoani Kigoma, huku ikiwataka wafanyabiashara kutumia maonesho ya biashara kama fursa ya kutangaza na kukuza shughuli zao.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dennis Londo,kabainisha hayo wakati akifungua maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Lake Tanganyika (Lake Tanganyika International Expo 2026) yanayofanyika katika viwanja vya Mwanga Community Center Mkoani humo.

Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Denis Londo akizungumza na wafayabiashara wakati akikagua mabanda ya maonesho Mjini Kigoma( Picha na Tryphone Odace).

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa amesema Mkoa huo unaendelea kujipambanua kuwa kitovu cha biashara kutokana na fursa mbalimbali zilizopo huku akiwataka wafanyabiashara kuzitumia fursa hizo kwa manufaa ya biashara na uchumi wa Mkoa.

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dkt. Rashid Chuachua aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo katika ufunguzi wa maonesho hayo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya biashara na uwekezaji nchini.

Kwa upande wake Balozi wa Ubalozi Mdogo wa Burundi Mkoani Kigoma, Kekenwa Jeremiah amesema maonesho hayo yamekuwa jukwaa muhimu la kukutanisha watu kutoka tamaduni mbalimbali pamoja na kutoa fursa kwa wafanyabiashara kubadilishana uzoefu na mawazo yanayoweza kuchochea maendeleo.

Maonesho hayo ya Kimataifa ya biashara yanatarajiwa kuhitimishwa kesho yakishirikisha wafanyabiashara kutoka mataifa mbalimbali, yakiwemo Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Tanzania.

Naibu Waziri wa biashara na viwanda akikagua mabanda ya maonyesho Mjini Kigoma, Picha na Tryphone Odace.

Wafanyabiashara hao wanaendelea kuonesha bidhaa mbalimbali, zikiwemo za viwandani, kilimo, biashara na bidhaa zinazobeba utamaduni wa Mataifa yanayoshiriki maonesho hayo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.