Katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya kwa wakati na bila vikwazo, Serikali imeendelea kutoa Kadi za Bima ya Afya kwa Wote kwa wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) wa Manispaa ya Singida.
Kadi hizo zimetolewa kwa wanufaika wa TASAF katika Kata ya Mwankonko, Manispaa ya Singida, wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, aliyekuwa akizungumza na wananchi wa eneo hilo.
Dendego alisema hatua hiyo ni sehemu ya dhamira ya Serikali ya kuhakikisha wananchi, hususan wazee na kaya zenye uhitaji, wanapata huduma muhimu za afya bila vikwazo.
Alisema Serikali imeendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kuboresha upatikanaji wa huduma za afya, hasa kwa wananchi wanaoishi maeneo ya pembezoni, ili waweze kupata matibabu kwa urahisi na kwa wakati.
Aidha, alisema Mkoa kwa kushirikiana na Serikali utaendelea kuhakikisha huduma muhimu zinapatikana katika maeneo ya pembezoni, ikiwemo upatikanaji wa magari ya wagonjwa (ambulance).
Discussion
Reader comments
0 contributions