Na Saulo Stephen - Singida.
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka Watanzania kuchukua tahadhari na kujiandaa mapema kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya El Niño, hususan mafuriko katika maeneo hatarishi.
Dkt. Mwigulu amezungumza hayo Septemba 6, 2026, wakati akiongea na wananchi wa Jimbo la Ilongero, Wilaya ya Singida, mkoani Singida, ambapo amesisitiza umuhimu wa kutambua mapema maeneo yenye historia ya mafuriko na kuchukua hatua za kinga kabla ya mvua hizo kuanza.

Amesema wananchi wanaoishi katika maeneo yanayofahamika kuwa hatarishi wanapaswa kuzingatia taarifa na maelekezo ya mamlaka husika, huku akisisitiza umuhimu wa kuepuka kujenga au kuishi katika maeneo yanayoweza kuathiriwa na mafuriko.
Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kujiandaa kukabiliana na athari za mvua hizo kwa kuimarisha uwezo wa kukabiliana na mafuriko, ikiwemo kuwa na vifaa na magari ya kuchimba mabwawa katika kila ukanda, huku akisisitiza kuwa maandalizi ya mapema ni muhimu katika kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.


Discussion
Reader comments
0 contributions