Skip to main content

SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA MPANGO WA ELIMU JUMUISHI NCHINI

Katika kuendelea kuboresha elimu nchini, Serikali imezindua Mkakati wa Taifa wa Elimu Jumuishi, miongozo na vifaa vya kielimu saidizi vya kidijitali kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA MPANGO WA ELIMU JUMUISHI NCHINI
Studio Narration JAMBO FM

SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA MPANGO WA ELIMU JUMUISHI NCHIN...

0:00 --:--

Katika kuendelea kuboresha elimu nchini, Serikali imezindua Mkakati wa Taifa wa Elimu Jumuishi, miongozo na vifaa vya kielimu saidizi vya kidijitali kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Uwekezaji huo unalenga kuongeza uwezo wa wanafunzi wenye mahitaji maalum kushiriki kikamilifu katika shughuli za kitaaluma na kukabiliana na vikwazo vinavyoathiri ujifunzaji wao.

Uzinduzi huo umefanyika Oktoba 16, 2026 jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ambapo amesisitiza kuwa mikakati na vifaa hivyo visiwe nyaraka na vifaa vya kuonesha mafanikio pekee, bali viwe nyenzo za kuleta mabadiliko halisi katika taasisi za elimu nchini.

"Serikali imewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 12 katika kuboresha miundombinu ya shule jumuishi za mfano, majengo na shule kongwe za elimu maalum, pamoja na kuwezesha mafunzo kwa watumishi 2,058 wakiwemo walimu wa elimu maalum 1,276, walimu wenye ulemavu 242, pamoja na walezi na mawakala 316,"amesema.

Aidha, amewataka viongozi wa taasisi kuhakikisha uwekezaji huo unaofanywa na Serikali kuhakikisha unaleta matokeo yaliyokusudiwa.

"Watumishi wafahamu na kutekeleza miongozo hiyo, walimu na wakufunzi wajengewe uwezo unaohitajika na mifumo ya ufuatiliaji na tathmini itumike kupima matokeo yake," amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Husna Sekiboko amewataka wanafunzi wenye ulemavu kujiamini na kutumia vifaa saidizi walivyopatiwa katika kuboresha masomo yao huku akiwasisitiza kuwa ulemavu si kikwazo cha kufikia mafanikio.

"Wanafunzi wakitumia vifaa hivi kwa usahihi, wakajituma katika masomo na kujiwekea malengo, wanaweza kufikia nafasi mbalimbali za uongozi na kutoa mchango mkubwa kwa taifa,"amesema.

Awali akitoa taarifa kuhusu vifaa hivyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema vifaa hivyo vina thamani ya Shilingi milioni 200, vikiwemo kompyuta mpakato 200 na tableti 240 ambapo vitasaidia kuboresha mawasiliano, upatikanaji wa taarifa na ushiriki katika shughuli za ufundishaji na ujifunzaji.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.