Skip to main content

SERIKALI YAANZA KUIMARISHA MAANDALIZI MADHARA YANAYOWEZA KUSABABISHWA NA MVUA ZA EL-NINO

Na Gideon Gregory - Dodoma.

SERIKALI YAANZA KUIMARISHA MAANDALIZI MADHARA YANAYOWEZA KUSABABISHWA NA MVUA ZA EL-NINO

Na Gideon Gregory - Dodoma.

Serikali imeanza kuimarisha maandalizi ya kukabiliana na madhara yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba mwaka huu, wakati wataalamu wa hali ya hewa wakionya kuwa kuimarika kwa hali ya El Niño kunaweza kuongeza mvua katika maeneo kadhaa ya Ukanda wa Pembe ya Afrika.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Septemba 2,2026 Jijini Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu), Prof. Paramagamba Kabudi amesema ofisi hiyo imeratibu maandalizi ya Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kukabiliana na Madhara ya El-Niño kwa kutenga kiasi cha shilingili bilioni 730 za dharura.

Kwa mujibu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), Oktoba hadi Desemba ni kipindi muhimu cha mvua katika maeneo ya ikweta na kusini mwa Ukanda wa Pembe ya Afrika, ambapo mvua za kipindi hicho zinaweza kuchangia hadi asilimia 70 ya mvua zote za mwaka katika baadhi ya maeneo ya Ethiopia, Kenya na Somalia, na hadi asilimia 40 katika baadhi ya maeneo ya Tanzania, Rwanda, Burundi na Uganda.

Utabiri wa kikanda, unaonesha pia uwezekano mkubwa wa mvua za msimu kuzidi milimita 400 katika baadhi ya maeneo ya katikati hadi kusini mwa Somalia, maeneo ya kati ya Kenya na magharibi mwa Tanzania. 

Prof. Kabudi amesema, El Niño inayotarajiwa mwaka 2026 inaweza kuwa kubwa na kufanana na El Niño iliyowahi kutokea nchini mwaka 1950.

Amesisitiza pia umuhimu wa wananchi kupata na kuzingatia taarifa za tahadhari zinazotolewa na mamlaka husika, huku akivitaka vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara yanayoweza kujitokeza, umuhimu wa maandalizi na hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

Ikumbukwe kuwa Agosti 18, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitoa utabiri wa Msimu wa Vuli ambao ulieleza uwepo wa Hali ya El-Niño yenye nguvu itakayopelekea mvua kubwa zitakazoweza kusababisha mafuriko.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.