Skip to main content

SERIKALI, WADAU WAJADILI CHANGAMOTO BIASHARA MAKAA YA MAWE

Na Gideon Gregory - Dodoma.

SERIKALI, WADAU WAJADILI  CHANGAMOTO BIASHARA MAKAA YA MAWE

Na Gideon Gregory  - Dodoma.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amekutana na wadau wa sekta ya makaa ya mawe wakiwemo wachimbaji na wafanyabiashara katika kikao maalum kilicholenga kujadili changamoto na fursa zilizopo katika biashara hiyo muhimu kwa uchumi wa nchi.

Akizunguza katika kikao hicho leo Machi 30,2026 Waziri Mavunde meielekeza Tume ya Madini kutotangaza bei elekezi ya makaa ya mawe bila kushirikisha wadau wa sekta hiyo.

Amesema hatua hiyo ni muhimu ili kuhakikisha bei hizo zinaendana na uhalisia wa soko la dunia na kulinda maslahi ya wachimbaji, wasafirishaji pamoja na uchumi wa nchi kwa ujumla.

Pia, amewahimiza  wadau kuanzisha umoja wao utakaosaidia kuwasilisha kwa pamoja maslahi yao na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya sekta hiyo.

Awali, wadau hao, wakiwemo viongozi wa juu wa baadhi ya makampuni ya makaa ya mawe nchini, wameeleza changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika sekta hiyo.

Ambapo wamesema,miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na bei elekezi zisizoendana na hali halisi ya soko, makato ya mrabaha, pamoja na uwepo wa baadhi ya wafanyabiashara wanaounda makundi ya kupanga bei kwa pamoja kinyume na sheria.

Kwa upande wake, mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Sundi Malomo, alitumia fursa hiyo kueleza taratibu zinazotumika katika upangaji wa bei za madini, akisisitiza umuhimu wa kuzingatia miongozo iliyopo ili kuhakikisha uwazi na usawa katika sekta hiyo.

Kikao hicho kinatajwa kuwa hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi, huku matarajio yakiwa ni kuongeza mchango wa makaa ya mawe katika pato la taifa na ajira kwa Watanzania.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.