Skip to main content

SERIKALI MANYONI YAHIMIZA USHIRIKIANO KUHARAKISHA MAENDELEO MAENEO YA WANANCHI

Na Saulo Stephen - Singida.

SERIKALI MANYONI YAHIMIZA USHIRIKIANO KUHARAKISHA MAENDELEO MAENEO YA WANANCHI
Studio Narration JAMBO FM

SERIKALI MANYONI YAHIMIZA USHIRIKIANO KUHARAKISHA MAENDELEO...

0:00 --:--

Na Saulo Stephen - Singida.

Wananchi Wilayani Manyoni, wametakiwa kujitolea na kushirikiana na Serikali katika kuharakisha maendeleo ya maeneo yao, huku wakihimizwa kutambua kuwa maendeleo ya kweli yanatokana na ushiriki wao wa moja kwa moja.

Rai hiyo imetolewa na Diwani wa Kata ya Manyoni Mjini, Stanley Mafanya, alipokuwa akifanya ziara katika Kitongoji cha Mlewa kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza pamoja na kutatua kero za wananchi.

Diwani wa Kata ya Manyoni Mjini, Stanley Mafanya.

Katika mkutano huo, wananchi waliwasilisha changamoto mbalimbali zikiwemo hitaji la kupatiwa elimu ya masuala ya ardhi, uwekaji wa mfumo wa anwani za makazi (Post Code) kwenye nyumba zao, pamoja na kupata ufafanuzi kuhusu taratibu za upatikanaji wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri.

Aidha, Afisa Lishe wa eneo hilo Sambu, aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha wanaunga mkono utoaji wa chakula cha lishe mashuleni, akieleza kuwa lishe bora huchangia afya njema na kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Naye Mtendaji wa Kata ya Manyoni, Simkonda, aliwahimiza wananchi kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa maeneo yao, akisisitiza kuwa usalama wa jamii huanza na ushiriki wa kila mwananchi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.