Rais Samia Suluhu Hassan, amesema kuhamia kwa Serikali Dodoma kumechochea ukuaji wa jiji hilo, kuongeza idadi ya watu, shughuli za biashara, uwekezaji na huduma mbalimbali.
Amesema hatua hiyo imefungua fursa za kiuchumi na kijamii, huku wananchi wakinufaika na ongezeko la maduka ya vifaa vya ujenzi na vituo vya huduma.

Amesema Serikali, sekta binafsi na wananchi wameongeza ujenzi wa majengo ya kisasa ya makazi, biashara na utoaji wa huduma mbalimbali.
Rais Samia ameyasema hayo leo, Oktoba 30, 2025, wakati wa uzinduzi wa Mji wa Serikali Mtumba.
Discussion
Reader comments
0 contributions