Skip to main content

SERIKALI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA VIONGOZI WA DINI UTOAJI ELIMU UMUHIMU WA KULINDA AMANI

Na Faustine Kasala - Kigoma.

SERIKALI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA VIONGOZI WA DINI UTOAJI ELIMU UMUHIMU WA KULINDA AMANI

Na Faustine Kasala - Kigoma.

Imeelezwa kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa dini zote katika kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kulinda Amani ya nchi yao na kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuhusiana na matukio yote yenye kuashiria uvunjifu wa amani.

Akizungumza katika kongamano la maombi kwa ajili ya viongozi wa nchi na Taifa kwa ujumla yaliyoandaliwa na Kanisa la Mji wa Makimbilio lililopo Stendi Mpya Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma, Mwakilishi wa Serikali Gama A Gama amesema elimu inayoendelea kutolewa kupitia majukwaa mbalimbali yakiwemo yale ya Dini Serikali itaendelea kuyaunga mkono kwani suala la kulinda usalama wa nchi ni la kila raia.

''Ushirikiano kati ya viongozi wa dini na Serikali unazidi kuimarika siku hadi siku na hiki kilichofanyika leo katika kanisa hili la Mji wa Makibilio kutoa nafasi kwa waumini wake kuliombea amani Taifa lao na kuwakumbusha umuhimu wa kulinda amani ya nchi ni jambo jema mno, na ninaamini sasa wanakwenda kuwa mabalozi wazuri wa Amani ya Taifa lao huko mtaani"Alisema Gama

Kwa upande wake Kiongozi wa Kanisa hilo Mtume Cristopher Kibami amesema ni jukumu la viongozi wa dini kuwaombea viongozi wa nchi ili waweze kuwatumikia wananchi kwa amani na utulivu.

''Katika kuhubiri kwetu tunasema Mamlaka yote hutoka kwa Mungu, hivyo kutokuheshimu viongozi nikupingana na neno la Mungu,tuwaheshimu viongozi wetu, tuwaombeeni viongozi wetu ili watawale kwa amani,tusiwasumbue tukifanya hivyo hawezi kuwaza maendeleo kwa wananchi na badala yake watawaza kupambana na wanaowasumbua"Alisema Mtume Kibami

Nao baadhi ya waumini wa Kanisa hilo walioshiriki Kongamano hilo Labona Mkungu na Lazaro Selemani wamesema Kongamano hilo limekuwa ni la baraka kwao na zaidi wamejifunza umuhimu wa kuwaombea baraka kwa Mungu viongozi wa nchi, kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu kwa lengo la kudumisha amani ya Nchi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.