Skip to main content

SAKATA LA UWANJA ARUSHA: MSIGWA NA WENZAKE WALITAKIWA KUWA GEREZANI - WAITARA

Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara, amesema wote waliohusika katika mchakato wa ujenzi wa Uwanja wa mpira wa Arusha, akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, walipaswa kuchukuliwa hatua za kisheria, ikiwemo kufungwa jela.

SAKATA LA UWANJA ARUSHA: MSIGWA NA WENZAKE WALITAKIWA KUWA GEREZANI - WAITARA
Studio Narration JAMBO FM

SAKATA LA UWANJA ARUSHA: MSIGWA NA WENZAKE WALITAKIWA KUWA G...

0:00 --:--

Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara, amesema wote waliohusika katika mchakato wa ujenzi wa Uwanja wa mpira wa Arusha, akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, walipaswa kuchukuliwa hatua za kisheria, ikiwemo kufungwa jela.

Waitara ameyasema hayo leo, Novemba 4, 2026, Bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia mjadala kuhusu ongezeko la gharama za ujenzi wa uwanja huo kutoka Bilioni 187 - Bilioni 338.

Waitara pia amehoji sababu zinazotolewa kuhusu ongezeko la gharama, ikiwemo maelezo yanayohusisha mabadiliko hayo na maelekezo ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

"Kama Bunhe lingekuwa linawajibisha ipasavyo, waliohusika katika maamuzi ya matumizi ya fedha za mradi huo wanapaswa kuwajibishwa," alisisitiza Waitara.

Amesema nchi inapitia wakati mgumu kiuchumi, hivyo ni muhimu kuhakikisha wote watakaobainika kuhusika na ubadhirifu au matumizi yasiyo halali ya fedha za mradi huo, wanafikishwa mahakamani.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.