Na Tryphone Odace - Kigoma.
Mahakama ya mwanzo ya Bangwe iliyopo Kata ya Bangwe Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani Kigoma, leo Augost 4, 2026, imemwachilia huru Mwenyekiti wa Mtaa wa Kisangani Abdallah Bwani Kimenya (69) baada ya kujiridhisha pasi na shaka kuwa mtuhumiwa hana hatia kutokana na shauri la jinai no 14/2026 lililokuwa linamkabili.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya mwanzo Bagwe Sylvester Milanzi amesema mshitakiwa alishitakiwa na mlalamikaji G3063 Innocent, ikiwa ni baada ya mshitakiwa kumdhamini Tumaini Jacob ambaye alikuwa na tuhuma za kuiba shilingi laki 800,000 mali inayomilikiwa na taasisi inayotoa mikopo aliyokuwa akiifanyia kazi.
Baada ya tuhuma hizo, Tumaini Jacob (Mwananchi) alikamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi Kigoma Mjini ambapo alimuomba Abdallah Bwani Kimenya (Mwenyekiti) kumdhamini na baada ya dhamana hiyo Abdallah Kimenya aliahidi kuwa kama Tumaini Jacob ikiwa atatoroka kabla ya kulipa kiasi cha fedha anachodaiwa atalipia kiasi cha shilingi laki 800,000.

Mnano Tarehe 13/7/2026 Abdalla Bwani Kimenya ambaye ni Mshitakiwa aliombwa kumpeleka kituo cha Polisi Ndugu Tumaini Jacob ambapo kwa makusudi hakumpeleka kituoni na kudai kuwa amekimbilia sehemu isiyojulikana.
Hivyo mshitakiwa akampelekwa Mahakamani kwa shitaka la kosa na kifungu cha sheria cha kutotii amri halali kifungu 124 cha kanuni ya Adhabu sura 16 chapisho la 2023.
Hata hivyo Mahakama baada ya kupokea shauri hilo mnamo tarehe 27/7/2026 na kusikiliza ushahidi kutoka pande zote imemwachia huru Abdallah Bwani Kimenya kwani hakuna ushahidi uliowasilishwa kuwa alikataa kulipa kiasi cha shilingi laki 800,000 ambayo aliahidi kwa Mkuu wa kituo cha Polisi OCS Kigoma kama hati ya dhamana.
Hapa kuwepo na amri halali iliyotolewa na Mkuu wa Kituo cha Polisi Kigoma Mjini OCS ya kukamatwa kwa Tumaini Jacob kwani Mlalamikaji katika kesi siyo mtu sahihi alitakiwa awe Mkuu wa kituo OCS Kigoma Mjini ambaye hajafungua kesi kama mlalamikaji anavyodai.
Mbali na hayo Mahakama hiyo imetoa rai kwa viongozi wa serikali za mitaa kujiepusha kuwadhamini wananchi wao, kwani wao ni viongozi na ni fedhea kushitakiwa mahakamani kutokana na makosa ya wananchi wao.
Discussion
Reader comments
0 contributions