Na Eunice Kanumba – Shinyanga.
Kufuatia Taarifa zilizoenea jana katika mitandao ya mbalimbali ya kijamii juu ya kukamatwa kwa wananchi katika kata ya Idukilo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga hatimae jeshi la polisi mkoani humo leo limetoa ufafanuzi juu ya sakata hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amesema wanawashikilia jumla ya watuhumiwa 75 ambao walihusika katika matukio mawaili ,tukio la kwanza Mei 28, 2026 katika kijiji cha Sanjo katika kata hiyo.
Mtendaji wa Kata, Masembe Mseni akiwa na Afisa Maendeleo Kata ya Mwadui, Lohumbo Rose Shao, Mwenyekiti wa kijiji cha Sanjo pamoja na wajumbe watatu wa serikali ya kijiji wakiwa katika zoezi la kuingiza kaya masikini kwenye mpango wa TASAF walivamiwa na watu waliokuwa na pikipiki mbili na kuanza kuwapiga kisha kuchana nyaraka walizokuwa wakifanyia kazi.

Baada ya hapo walisema hawataki kuona kiongozi yeyote wa seriakli anafanya kazi katika eneo hilo ambpo jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga baada ya tukio hilo lilianza upelelezi mara moja nakufanikiwa kuwakamata watuhumiwa waliohusika na tukio hilo.
Tukio la pili lilitokea June 1, 2026 majira ya saa sita na usiku katika kijiji cha Idukilo ambapo jeshi la polisi lilipata taarifa juu ya baadhi ya wanakijiji kuwapiga wanakijiji wenzao kwa madai ya kutoa siri za kijiji kwa jeshi la polisi na kwa mkuu wa wilaya ambapo walivunja baadhi ya maduka na kufanya uharibifu wa mali ambapo jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga lilifika na kuanza kufanya ukamataji wa wahalifu hao.
Akizungumzia chanzo hasa cha wananchi katika eneo hilo kufanya fujo hizo Kamanda magomi amesema kuwa hawataki viongozi wa kiserikali kufanya kazi katika eneo lao akiwemo diwani wa eneo hilo na viongozi wa kijji ambapo viongozi hao wakijiji wameshajiudhuru na kukimbia katika eno hilo
Akianisha hali ya usalama katika eneo hilo kamanda Magomi amesema inaendelea vizuri kwani jeshi la polisi lipo katika eneo hilo muda wote kuhakikisha ulinzi wa raia na mali zao huku likikemea vikali vitendo hivyo na kwamba kwa wale wote wanaohusika litahakikisha wanakamatwa na kufikishwa katika mkoano wa sheria.
Discussion
Reader comments
0 contributions