Na Afarah Suleiman - Dar es salam.
Wafanyabiashara wadogo wa Halmashauri ya mji wa Babati mkoani manyara, wameishukuru serikali kwa kuwawezesha kiuchumi kupitia mikopo ya asilimia 10 isiyo na riba, baada ya kufungua biashara zinazowaingizia kipato na kukidhi mahitaji yao ya kila siku.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 50 ya sabasaba jijini Dar es salaam, Afisa Biashara wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Upendo Ndile amesema, kupitia mikopo hiyo wajasiliamali wa Babati wamekuwa wanaufaika wakubwa kwa kujiendeleza kiuchumi.

Amewahimiza pia Wajasiriamali kuchangamkia fursa ya mikopo isiyo na riba, ili kuweza kukuza mitaji yao na kujiongezea kipato binafsi na familia kwa ujumla.


Discussion
Reader comments
0 contributions