Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza, SSP Sunday Ibrahim, amewataka wazazi, jamii, taasisi mbalimbali na madhehebu ya dini mkoani humo, kushirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha usalama wa watumiaji wote wa barabara unalindwa kikamilifu.
SSP Sunday ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye Kongamano la Maombi ya Watoto lililofanyika mkoani humo, likiwa na lengo la kuombea amani ya nchi na kumshukuru Mwenyezi Mungu.

Akitoa elimu ya usalama barabarani katika kongamano hilo, SSP Sunday amefafanua kuwa Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha usalama barabarani litaendelea kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya barabara kwa watoto na wazazi.
Amesema lengo ni kulinda haki zao za msingi, huku akisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi ya madereva wote wazembe na wale wanaokiuka kanuni, sheria na taratibu za usalama barabarani.



Discussion
Reader comments
0 contributions