Kiongozi wa upinzani Nchini Afrika Kusini, Julius Malema amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kufyatua risasi wakati wa mkutano wa hadhara nchini humo, miaka nane iliyopita.

Hukumu hiyo, inakuja kufuatia kesi ya Oktoba 1, 2025, ambapo mwanasiasa huyo alipatikana na hatia ya kumiliki silaha na risasi kinyume cha sheria, kufyatua silaha hadharani na kuhatarisha usalama wa watu.
Discussion
Reader comments
0 contributions