Skip to main content

RC SHIGELA ARIDHISHWA KASI UJENZI WA GHALA LA MSD GEITA

Na Ibrahim Rojala, Chato - Geita.

RC SHIGELA ARIDHISHWA KASI UJENZI WA GHALA LA MSD GEITA
Studio Narration JAMBO FM

RC SHIGELA ARIDHISHWA KASI UJENZI WA GHALA LA MSD GEITA

0:00 --:--

Na Ibrahim Rojala, Chato - Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametembelea, kukagua na kuelezea kuridhishwa na kasi ya  ujenzi wa ghala la Bohari ya Taifa ya Dawa (MSD) na ofisi unaotekelezwa na serikali wilayani Chato Mkoani Geita kwa thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 19.

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo Mei 19, 2026, RC Shigela ameeleza kwamba ni matumaini yake kwamba mradi  utakamilika mwezi Oktoba mwaka huu ili kukamilisha dhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha dawa zinapatikana kutoka katika ofisi hizo ambazo zinatarajiwa kuhudumia mikoa ya Kagera,Shinyanga na Kigoma.

‘Mkandarasi hana kisingizio,fedha anazo,hana kisingizio wataalamu wa kujenga wapo,hana kisingizio,vifaa amesema mobilization asilimia 100%,tunatarajia Oktoba jingo hili na ghala hili litakamilika’’amesema RC Shigela

Mhandisi msimamizi kutoka kwa Mkandarasi anayesimamia utekelezaji wake,Patrick Laibo ameeleza kwamba mradi huo ulianza kutekelezwa Agosti 20,2025 matarajio ya kukamilika kwake yakiwa ni Oktoba 19,2026 ukihusisha ujenzi wa ghala na ofisi za MSD na kubainisha kwamba mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 57.

“Kwa maana yo ofisi,ghala na miundombinu ya nje ambayo kuna tenki la maji,chumba cha umeme pamoja na fensi ambavyo viko almost asilimia 90% kwa external facilities, kwa upande wa ghala peke yake lina asilimia 48%, kwa upande wa ofisi tuko asilimia 60% ameeleza Mhandisi Laibo

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Chato, Barnabas Nyerembe,ameelezea kushuhudia mabadiliko katika utekelezaji wa mradi huo ikilinganishwa na hali waliyoikuta walipokagua mradi huo wakiwa na kamati ya siasa na halmashauri kuu ya wilaya na kuwapongeza wakandarasi kwa namna wanavyoendelea na utekelezaji wa mradi huo.

Nae Diwani wa Kata ya Chato, Mange Ludomya,ameeleza kuwa miongoni mwa faida wanazotarajia kuzipata baada ya kukamilikakwa mradi huo kuwa ni pamoja na mwingiliano wa watu kiuchumi na kijamii na kuishukuru serikali kwakuendelea nautekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya wilaya ya Chato.

Wakati huo huo kupitia ziara hiyo,Mkuu wa Mkoa wa Geita,Martine Shigela amekabidhi injini ya boti yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tano kwa kikundi Kambale Group kinachojihusisha na ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba katika kijiji cha Lubambangwe wilayani Chato mkoani Geita.

Injini hiyo imetolewa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi. Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa aliyoitoa kwa kikundi hicho baada ya kuelezwa uwepo wa changamoto ya boti yakupeleka chakula,na kufanyia doria za ulinzi katika vizimba.

‘Leo nimekuja hapa kama sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwa Waziri wetu wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Bashiru Ally, kuwawezesha wavuvi wetu tayari boti ile imeshanunuliwa kwa zaidi ya milioni tano na laki nne,Mheshimiwa Waziri ametoa fedha nyingi, zilipopungua pungua kidogo Mheshimiwa Magembe akaongezea na Mheshimiwa Lutandula akaongezea na boti sasa imekamilika iko hapa na leo nawakabidhi wanakikundi tuweze kuitumia kwa maendeleo yetu,’ ’ameeleza.

Kupitia taarifa ya kikundi cha Kambale Group kilichonufaika na msaada wa injini hiyo ilioyosomwa mbele ya mkuu wa Mkoa wa Geita,imeelezwa kwamba awali kikundi husika kilinufaika na mkopo mkopo wa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 91 kupitia wizara ya mifugo na uvuvi,fedha zilizowezesha utekelezaji wa mradi wa vizimba vitano vya chuma,chakula,na vifaranga vya samaki hatua iliyowezesha kikundi hicho kuvua zaidi ya tani 6 za samaki.

Kupitia hafla hiyo, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Chato, Barnabas Nyerembe amekitaka kikundi hicho navingine kuwahusisha wataalamu katika utekelezaji wa miradi yao akiwataka maafisa uvuvi na maafisa ushirika kukisaidia kikundi hicho baada ya kubaini kuwa kikundi hicho kimeuza samaki wote na kutokuwa na vifaranga vya samaki hali inayoathiri mwenendo wa mradi

‘Mna haja ya kufanya chochote mnachofanya lakini mkabaki na mtaji kwaajili ya kazi yenu iendelee,niwaombe sana mzingatie hili,sisi wakulima tunapokuwa tumetoa mavuno shambani huwa tunakuwa waangalifu sana kutunza mbegu’amesema Nyerembe

Akizungumza kuhusu mafanikio ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba, Afisa Uvuvi wilaya ya Chato, Avodia Sylvester amesema awali walianza na kizimba kimoja kabla ya wafugaji kuongezeka hadi kufikia vikundi vitano,watu binafsi 12, idadi ya vizimba vilivyosajiliwa vikiwa 43.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.