Skip to main content

RC MTAMBI ATAKA ULINZI WA RASILIMALI ZIWA VICTORIA

Na Adam Msafiri - Mara.

RC MTAMBI ATAKA ULINZI WA RASILIMALI ZIWA  VICTORIA

Na Adam Msafiri - Mara.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi ameagiza Kamati ya Usalama ya Mkoa huo, kuhakikisha inachukua hatua kali dhidi ya watu wote watakaobainika kujihusisha na uvuvi haramu, huku akisisitiza kuwa serikali haitamvumilia mtu yeyote anayeharibu rasilimali za Ziwa Victoria.

Agizo hilo limetolewa Mei 28,2026 wakati wa uzinduzi na kukabidhi vizimba 40 vya ufugaji samaki kwa vijana wa programu ya Building a Better Tomorrow (BBT) mkoani Mara, mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 1.3 unaolenga kuwainua vijana kiuchumi kupitia sekta ya uvuvi.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kanali Mtambi amesema serikali imewekeza fedha nyingi kuwawezesha vijana kujiajiri hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kulinda rasilimali za maji na kuhakikisha shughuli za uvuvi zinafanyika kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.

“Jukumu la kuhakikisha ustawi wa Ziwa ni letu sote na wadau wote tunahusika,nizitake BMU’s kuendeleza umakini katika kukabiliana na uvuvi haramu lakini pia niitake Kamati ya Usalama ya mkoa kuhakikisha mnaongeza nguvu katika ulinzi wa Ziwa” amesema Kanali Mtambi.

Katika hatua nyingine, viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo wakiwemo wawakilishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,wameeleza namna mradi huo utakavyosaidia kuongeza ajira kwa vijana pamoja na kuchochea uchumi wa Mkoa wa Mara kupitia sekta ya uvuvi wa kisasa.

Mradi huo wa vijana 40 wa BBT umefadhiliwa kwa lengo la kuwawezesha vijana kujenga maisha bora kupitia uwekezaji katika ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba vya kisasa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.